Upekee wa samaki Kampango anayepatikana Ziwa Nyasa

Upekee wa samaki Kampango anayepatikana Ziwa Nyasa

Habari msomaji wetu wa magazine ya Mwananchi Scoop, tunatumai u mzima wa afya na unaendelea vema na masomo yako hapo chuoni na kwa waliomakazini nanyi mnawajibika ipasavyo.

Basi leo katika kipengele cha listi tumekosogezea baadhi ya vitu ambavyo vinafanya samaki Kampango kuwa wa pekee kati ya samaki wote wanaopatikana Ziwa Nyasa.

Ziwa nyasa ni miongoni mwa maziwa matatu makubwa yanayopatikana Kusini mwa Afrika na Afrika Mashariki, neno nyasa limetokana na lugha ya chichewa (malawi) ikiwa na maana ya ziwa. Ziwa Nyasa ni ziwa la nane kwa ukubwa duniani na la tatu kwa kina kirefu kuanzia 264-700M.

Ziwa hili linatumika na nchi tatu yaani Malawi, Tanzania na Msumbiji, ikiwa sehemu kubwa ipo nchini Malawi. Ziwa Nyasa lina ukubwa wa 29600km2 lenye maji safi (fresh water).Lina  jamii ya samaki zaidi ya 1000 na sifa kubwa lina asilimia tisini na tano (95%)  ya samaki ambao wanapatikana ziwa hili tu ni ( ziwa lenye endemic species  wengi duniani.

Ajabu ya maji ya ziwa Nyasa ni kuwa juu yana hali ya joto (24-29) lakini sehemu ya chini (bottom) maji ni baridi (22), hali hii ya utengano wa jotoridi la maji (thermocline) hutokea kuanzia kina 40-100M.

 

Samaki wapo wa aina nyingi wakiwepo (cichlid na non- cichlid), kambare, tilapia akiwepo na kampango (bagrus meridionalis). Pia ziwa hili hupokea maji kutoka katika mito mingi kama vile vile mto Ruhuhu, Songwe na Dwangwa.

Zijue sifa samaki kampango

Ndugu msomaji pengine umewahi kufika ziwa Nyasa (wilaya ya Nyasa mkoa wa Ruvuma) au wilaya ya Kyela, je, umewahi kumuona samaki anaitwa Kamapango (scientific name: bagrus meridionalis). 

Jina Kampango ni jina la asili samaki huyu anapatikan ziwa Nyasa tu na ana sifa kubwa sana ambayo pengine umewahi kuona au kusikia kwa viumbe wengine.

Hebu tuone bagrus meridionalis au Kampango kama anavyofahamika na wengi ana sifa zipi ambazo zinampa upekee wake katika ziwa Nyasa na jamii ya Kampango.

Samaki kampango (bagrus meridionalis)

Ni samaki pekee wanaolea watoto wao kwa pamoja yaani baba na mama mpaka wafikie 12cm (wakubwa). (biparental care).  Jee ni samaki gani mwingine huwa anafanya hivi? (Basi kama una mfahamu  toa maoni  hapo chini)

Kampango hukua kufikia urefu wa 45cm kwa kawaida lakini pia hukua mpaka 1- 1.5M)

Samaki kampango akiwa na watoto.

Kampango huzaliana kipindi cha Januari mpaka Machi kila mwaka ambapo Kampango dume yeye hujenga kiota (nest) na jike hutaga mayai katika kiota. Mayai yasiyorutubishwa hutumika kama chakula kwa watoto baada ya kutotolewa, ambapo Kampango dume huenda kukamata wanyama wadogo wadogo (micro vertebrae or zooplankton) kwa ajili ya kuwalisha watoto wao Baba na mama wanahusika vema kuwalea watoto). Nukuu: Sifa ya kutumia mayai yake kama chakula pia awe na upekee sana.

Kampango hufanya mahusiano na viumbe wengine (mahusiano chanya,) kwamba yeye anauwezo wa kulinda mayai ya samaki wengine watakao kuja kutaga katika kiota chake na kulinda mayai mpaka watoto wakue.

Lakini pamoja na hayo yale mayai ambayo hayata rutubishwa hutumika kama chakula kwake na watoto wake.(brood parasitism).

Kampango hupatikana sana usiku au anaweza kufanya kazi sana usiku katika kujitafutia chakula (nocturnal). Hupendelea sana kwenye mapango ya mawe, sehemu zenye matope, pia kina cha kawaida 50M ambapo Oksijeni inakuwa rahisi kupatikana.

 Vitisho dhidi ya samaki kampango

Samaki kampango ni miongoni mwa samaki waliopo hatarini kupungua au kupotea kwa sababu ya mambo yafuatayo;

Uvuvi haramu,

Uvunaji uliopitiliza,

Uchafuzi wa maji hivyo kupelekea kukosekana kwa hewa safi kwenye maji.

Imeandaliwa na Janeth Jovin kwa msaada wa Wildlife Tanzania.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post