Peter Akaro
Usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Peacock huko Los Angeles, Calfornia nchini Marekani kumetolewa tuzo za BET 2024 ambapo Usher Raymond IV na Tyla ndio mastaa waliong'aa zaidi.
Tuzo hizi zinazoandaliwa na Black Entertainment Television (BET), tangu Juni 19, 2001 zinalenga kusheherekea mafanikio ya kazi za Wamarekani Weusi katika sanaa ya muziki, uigizaji na michezo.
Hata hivyo, mwaka 2010 BET walianza kujumuisha wasanii wa Afrika katika tuzo hizo kupitia kipengele cha 'Best International Act; Africa' ambacho 2018 kilibadilishwa na kuwa 'Best International Act' kikihusisha wasanii wote kutoka nje ya Marekani.
Usher amepokea tuzo ya Heshima ya Mafanikio katika Sanaa, pia ameshinda kama Msanii Bora wa Kiume wa R&B/Pop kwa mara ya tano akiwa ni msanii wa pili aliyeshinda kipengele hicho mara nyingi zaidi nyuma ya Chris Brown aliyeshinda mara saba.
Kwa upande wake Tyla kutoka Afrika Kusini ambaye pia mshindi wa Grammy 2024, ikiwa ni mara yake ya kwanza kuwania BET ameshinda tuzo mbili sawa na Victoria Monet.
Tyla ameshinda kama Msanii Bora Kimataifa akiwabwaga Asake (Nigeria), Aya Nakamura (Ufaransa), Ayra Starr (Nigeria), Bk’ (Brazil), Cleo Sol (Uingeza), Focalistic (Afrika Kusini) na Karol Conka (Brazil).
Vilevile Tyla aliyetamba na wimbo wake, Water (2023), ameshinda kama Msanii Bora Chipukizi mbele ya 41, 4Batz, Ayra Starr, Bossman Dlow, Fridayy, October London na Sexyy Red.
Kwa matokeo hayo, Tyla anakuwa msanii wa tatu ambaye hakuzaliwa Marekani kushinda kipengele cha Msanii Bora Chipukizi, wengine ni Nicki Minaj aliyezaliwa Trinidad na Sam Smith aliyezaliwa Uingereza.
Msanii mwingine wa Afrika aliyeshinda ni Tems kutoka Nigeria aking'aa kipengele cha Wimbo Bora ya Injili/Uhamasishaji kupitia wimbo wake, Me & U (2023), hii inakuwa ni tuzo yake pili ya BET baada ya kushinda kama Msanii Bora Kimataifa 2022.
Naye Beyonce Knowles ameshinda kipengele cha Chaguo la Watu kupitia wimbo wake, Texas Hold ’Em (2024), hii inakuwa tuzo yake 33 na kuendelea kuwa msanii aliyeshinda tuzo nyingi zaidi za BET kwa muda wote akifuatiwa na Chris Brown aliyeshinda tuzo 19.
Orodha kamili ya washindi wa BET 2024 hii hapa chini.
Album of the year
Killer Mike, Michael — Mshindi
Best female R&B/pop artist
SZA — Mshindi
Best male R&B/pop artist
Usher — Mshindi
Best group
¥$, Ye, Ty Dolla $ign — Mshindi
Best collaboration
Lil Durk feat. J. Cole, “All My Life” — Mshindi
Best female hip-hop artist
Nicki Minaj — Mshindi
Best male hip-hop artist
Kendrick Lamar — Mshindi
Best new artist
Tyla — Mshindi
Video of the year
Victoria Monét, “On My Mama” — Mshindi
Video director of the year
Cole Bennett — Mshindi
Dr. Bobby Jones Best Gospel/Inspirational Award
Tems, “Me & U” — Mshindi
Viewer’s choice award
Beyoncé, “Texas Hold ‘Em” — Mshindi
Best international act
Tyla (Africa) — Mshindi
Viewer’s choice: Best new international act
Makhadzi (Africa) — Mshindi
BET Her
Victoria Monét, “On My Mama” — Mshindi
Best movie
Bob Marley: One Love — Mshindi
Best actor
Denzel Washington — Mshindi
Best actress
Regina King — Mshindi
YoungStars Award
Blue Ivy Carter — Mshindi
Sportswoman of the Year Award
Angel Reese — Mshindi
Sportsman of the Year Award
Jalen Brunson — Mshindi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply