Twiga mweupe anayelindwa nchini Kenya

Twiga mweupe anayelindwa nchini Kenya

Twiga pekee mwenye rangi mweupe duniani anapatikana Kaskazini Mashariki ya Kenya Garissa, amefungwa kifaa maalumu cha kufuatilia mienendo yake ya kila siku ili kumlinda dhidi ya maharamia ambao wanadaiwa kuwa tayari wameshaua twiga wawili wa aina hiyo.

Twiga huyo ambaye jinsia yake ni ya kiume amekuwa mweupe kwa sababu ya upungufu wa kimaumbile ambao kitaalamu huitwa 'leucism',  husababisha kupoteza rangi katika ngozi.

Twiga wawili ambao waliuawa Machi mwaka 2020, nao walikuwa na rangi kama yake hivyo kwa sasa yeye ndiyo amebakia kuwa twiga mweupe pekee duniani.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post