Unapozungumzia muziki wa Bongo Flava kwenye jukwaa la kimataifa, ni jina moja tu litatajwa nalo ni Diamond Platnumz, yeye si nyota tu ni sura ya muziki wa Kitanzania, ambaye amejikita zaidi katika kuutambulisha muziki wa Bongo Fleva duniani.
Wakati wasanii wengi wakiendelea kupaa, hakuna aliyefanikiwa kuvunja mipaka ya kimataifa kama Diamond anavyofanya.
Siri ya mafanikio yake makubwa inaelezwa kuwa ni ya kipekee huku ikichagizwa zaidi na kujifunza kila siku, kupataa maarifa mapya pamoja na kuelewa radha wanayoihitaji mashabiki.
Kupitia mahojiano yake ya hivi karibuni na Trace, Diamond alieleza kuwa kujifunza mambo mapya ndio siri ya mafanikio yake.
“Ili msanii kudumisha hadhi yake, lazima ajifunze mambo mapya kila siku kwa sababu dunia inabadilika kila wakati, nilipoanza muziki wangu ulikuwa wa tofauti sana”, alisema Diamond
Kadri muda unavyozidi kupita sauti ya msanii huyo inazidi kubadiliki kutoka kuimba ‘Kamwambie’ na ‘Number One’ na sasa amejikita katika ladha ya Amapiano kama ‘Komasava’ alifuunguka na kueleza kuwa sasa anaweza kufanya aina yoyote ya muziki.
“Sasa, naweza kufanya aina tofauti za muziki naweza kujaribu chochote, iwe ni Amapiano au kitu kingine,” alisema.
Wakati wasanii wengi wakikwama kwenye mtindo mmoja, uwezo wa Diamond wa kuendana na mabadiliko na kuvumbua njia mpya za kufanikiwa anadai kuwa si rahisi kujifunza vitu vipya kila siku bali ni kukubali changamoto za kushindwa.
“Si rahisi, kusema kweli, Lakini ukijifungua kujifunza na kukua, kila kitu kinawezekana, Sijali nikikosea. Kadri ninavyokosea, ndivyo ninavyoboresha”, amefunguka Diamond
Leave a Reply