Kibongo Bongo kuomba chumvi au kiungo chochote wakati wa chakula kwa lengo la kuongeza radha jambo hilo huchukuliwa la kawaida na halina shida yoyote, lakini unapoingia nchini Misri jambo hilo hutafsiriwa kama dharau kwa aliyeandaa chakula hicho.
Kwa mujibu wa tovuti ya “Click For Translation” Nchini Misri kuomba chumvi au kiungo chochote wakati wa chakula kitendo hicho kinachukuliwa kama kosa kubwa na tusi kwa mwenyeji wako aliyekuandalia chakula.
Misri chakula huchukuliwa kama zawadi kutoka kwa Mungu na kielelezo cha ukarimu, unapoalikwa kwa ajili ya mlo nyumbani kwa mtu inachukuliwa kuwa si adabu kuomba chumvi au kiungo kingine chochote kwani inamaanisha haukithamini chakula kilichotayarishwa kwa ajili yako.
Hii inatokana na watu wa nchi hiyo kusifika kwa kutumia viungo vingi katika vyakula vyao hivyo basi wanaamini kuwa wanapopika chakula basi huwa wanaweka viungo sawa kwenye vyakula wanavyoviandaa na wala hakuna haja ya mlaji kuongeza kiungo chochote.
Ni muhimu kukumbuka kwamba desturi na adabu za chakula zinaweza kutofautiana sana kutoka tamaduni moja hadi nyingine, wewe Kama mgeni kwenye jamii hiyo ni jukumu lako kuheshimu mila na desturi za tamaduni unayotembelea na kuepuka tabia yoyote inayoweza kusababisha kero au dharau kwa wenyeji wako.
Leave a Reply