Jake Paul ashinda pambano dhidi ya Tyson

Jake Paul ashinda pambano dhidi ya Tyson


Waswahili wanasema usiku wa deni haukawii kukucha, basi msemo huu unajidhihirisha kufuatia na pambano ambalo lilisubiriwa kwa hamu la bondia wa zamani wa ngumi za kulipwa Mike Tyson na Jake Paul, ambapo bondia Jake alishinda pambano hilo kwa pointi.

Pambano hilo la raundi nane lilifanyika katika Uwanja wa AT&T huko Arlington, Texas na kukamilika kwa matokeao ya pointi 80-72 na 79-73 huku likimfanya bondia Jake kuinuka kidedea katika mtanange huo.

Awali pambano hilo lilipangwa kufanyika Julai 20 katika uwanja huo huo pamoja na kuoneshwa moja kwa moja (live) katika mtandao wa Netflix, lakini lilihairishwa baada ya Tyson kupata matatizo ya kiafya.

Jake Paul amekuwa na mafanikio kadhaa katika mchezo huo, na kupitia rekodi yake ameshawahi kuwashinda nyota wa zamani wa UFC kama Nate Diaz, Anderson Silva, Tyron Woodley, Andre August, Bourland na sasa ameongeza listi kwa kumchapa Tyson.

Utakumbuka kuwa mara ya mwisho Tyson ambaye ni bingwa wa zamani wa uzito wa juu kuingia ulingoni ilikuwa ni mwaka 2020, ambapo lilikuwa ni pambano la raundi nane dhidi ya Roy Jones Jr lililofanyika jijini Los Angeles huku pambano hilo likitamatika kwa suluhu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags