Maua Sama atuma salamu za pole Kariakoo

Maua Sama atuma salamu za pole Kariakoo

Mwanamuziki anayetamba na kiboa cha ‘Kariakoo’ ametuma salamu za pole kwa wafanyabiashara wa Kariakoo kufuatia na tukio lililotokea mapema leo la kuporormoka kwa moja ya jengo katika eneo hilo.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Maua ameshare kava ya wimbo wa ‘Kariakoo’ ukiwa na ujumbe wa salamu za pole huku akiwaombe majeruhi Mungu awatie nguvu.

“Kwa niaba ya rafiki zangu G Nako, Ibraah na Jaiva ninawatakia pole wafanyabiashara wenzangu wa Kariakoo kufuatia tukio la kuanguka kwa jengo na kusababisha maafa kwa watu na biashara zao. Mungu awape nguvu waokoaji na majeruhi” ameandika Maua Sama

Utakumbuka kuwa Maua ana wimbo alioupa jina la Kariakoo ambao amewashirikisha wasanii wenzake ambao ni G Nako, Ibraah na Jaiva ambapo mpaka kufikia sasa wimbo huo unazaidi ya watazamaji 204,310 katika mtandao wa YouTube ukiwa na wiki mbili tu tangu kuachiwa kwake.

Watu kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha baada ya jengo la ghorofa lililopo Kariakoo Mtaa wa Masimbazi jijini Dar es Salaam kuporomoka, huku shughuli za uokoaji zikiendelea kufanyika katika eneo hilo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags