Shambulizi la Al-Shabaab laua watu wawili,Somalia

Shambulizi la Al-Shabaab laua watu wawili,Somalia

Watu wawili akiwemo mwanajeshi mmoja wamekufa katikati mwa Somalia kufuatia shambulio la kujitoa muhanga lililofanywa jana na kundi la kigaidi la Al-Shabaab, kundi lenye mafungamano na Al-Qaeda ambalo limekuwa likiendesha uasi dhidi ya taifa la Somalia kwa karibu miaka 15.

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amekabiliwa na ongezeko kubwa la harakati za Al-Shabaab tangu kuchaguliwa kwake mwezi Mei na ameahidi kuanzisha "vita" dhidi yao. Rais Joe Biden alisema atarejesha uwepo wa wanajeshi wa Marekani nchini Somalia ili kupambana na kundi hilo.

Licha ya kufurushwa kutoka miji mikubwa ya Somalia, ukiwemo mji mkuu Mogadishu mwaka 2011, Al-Shabaab inadhibiti maeneo ya mikoani na mara nyingi raia wamekuwa wakiathirika katika mapigano hayo.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post