Picha ya kihistoria na somo muhimu sana

Picha ya kihistoria na somo muhimu sana

Picha hii ilipigwa katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 1986. Pichani ni Maradona, Pele na Platini.

Maradona alikuwa balozi wa mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya. Platini alikuwa balozi wa mapambano dhidi ya ufisadi. Pele alikuwa balozi wa kusimamia haki za watoto.

Miaka michache baadaye Maradona akawa mraibu wa dawa za kulevya. Platini yeye alipigwa marufuku kwenye utawala wa soka kwa kashfa ya rushwa.

Na Pele alishitakiwa kwa kumkana bintiye wa kibaolojia, Sandra Regina Arantes, ambaye alizaliwa baada ya uhusiano wa kingono na dada wa kazi mwaka 1964.

Sandra alifungua kesi dhidi ya Pele. Na alishinda kesi hiyo baada ya vipimo vya DNA. Baadaye akaandika kitabu chake: "The Daughter The King Did Not Want".

 Ambacho kilielezea mapenzi ya mama na baba yake ambaye ndiye Mfalme wa Soka Duniani King Pele.

Mafunzo mawili muhimu:

  1. Hakuna mwanadamu aliyekamilika.
  2. Muonekano unaweza kukudanganya






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post