Pekosi habari ya mjini kwa sasa

Pekosi habari ya mjini kwa sasa

Pelagia Daniel

Pekosi ni aina ya suruali yenye muonekano unaoshika mwili kuanzia usawa wa kiuno hadi kwenye magoti wa juu lakini upande wa miguuni huachia kwa upana tofauti na suruali zingine zinazoshika mwili kuanzia juu hadi chini.
Katika historia ya mitindo Pekosi zilivaliwa sana kipindi cha miaka ya zamani hadi sasa na jinsi ya kike katika mitindo mbalimbali lakini likichukuliwa kama vazi la kawaida.

Ndipo ilipoingia fasheni ya skini jeans ambapo muundo wake hushika mwili kuanzia sehemu ya kiunoni hadi miguuni, mpaka leo nguo hizo zinavaliwa sana na jinsi ya kike na kubakia kuwa fasheni inayobamba.

Baada ya kuingia fasheni ya skin jeans watu walioendelea kuvaa Pekosi walionekana kama wamepitwa na fasheni hivyo kuufanya mtindo huo kutokuwa na thamani siyo kwa watoto wala wakubwa.

Kama Waswahili wanavyosema cha kale dhahabu msemo huo unajidhihirisha katika fasheni ya Pekosi, siku za hivi karibuni mtindo huo umerudi kwa kasi katika ulimwengu wa mitindo ukiwa wenye hadhi ya kifasheni pia kushika soko la biashara ya nguo. Thamani ya mtindo huo imekua kutokana na vazi hilo kuvaliwa sana na wasanii wa jinsi zote. Hivyo kutoa mwitikio chanya kwa watu wengine wanaoendana na trend ya fasheni kupata mwonekano wa kipekee.

Kwa sasa vazi hilo lipo katika namna mbili ile ya awali ikiwa na ubunifu wa rangi nzuri zinazovutia na ya pili mtindo wa kunakshiwa kwa mifuko mingi kuanzia juu mpaka sehemu za miguuni ikijulikana kama ‘Cargo jeans’ Jina lililotokana na fasheni hio ambayo ina mifuko unayoweza kuwekea vitu vingi kwa wakati mmoja bila kuathiri mwonekano wako.

Wanamitindo wanalizungumziaje vazi Hilo
Akizungumza na Mwananchi mbunifu wa mavazi, Tydo Master analizungumzia vazi la Pekosi kuwa limekuwa linabamba kutokana na namna lilivyochukua sura mpya bila kubagua jinsi tofauti na awali ambapo lilikuwa likivaliwa na wanawake tu. Anasema mtindo huo umebambakuanzia mwaka 2023 hadi sasa upo katika chati.

“Hili vazi lilikuwepo na kuna baadhi ya watu waliendelea kuvaa lakini mwaka 2023 lilibamba na kuingia katika chati ya mitindo hasa lilipovaliwa sana na watu maarufu nchini na wasanii. Zamani pekos iIlikuwa ilikuwa ikivaliwa na wanawake tu lakini sasa hivi kuna cargo jeans mtindo wa Pekosi inayovaliwa na jinsi zote” anasema Tydo

Pia Frivola mwenye brand ya Vola entire anaeleza namna unavyoweza kuvaa pekosi na kupata mwonekano wa kipekee. Pekosi huvaliwa na tisheti kubwa au saizi yako chini ukaivalia na raba kwa upande wa wanaume na wanawake unaweza kuvaa pekosi na crop top, vest, damini koti au tisheti kwa chini ukavaa sendo, croksi na raba. Utapata mwonekano mzuri wa kuvutia.

Wavaaji wamelipokeaje
Akizungumza na Mwananchi Aisha Mbuma anasema analizungumzia vazi la pekosi kupokelewa kwa mikono miwili hasa kwake kwa sababu anapenda kupendeza na kuendana na trend ya fasheni. Anaeleza pekosi humpa mwonekano unaovutia hasa akivaa na topu rangi isiyoendana na suruali hio.

“Raha ya kupendeza uendane na trend ya fasheni cha muhimu ikupendeze maana sio kila nguo inampendeza mtu. Pekosi hunipa mwonekano wa kipekee unaonifanya niwe nazo za rangi tofauti kama nne, nikiwa navaa huwa naivalia na topu za rangi tofauti na rangi ya suruali niliyoivaa” anasema Aisha






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post