MV Kazi yarudi kazini

MV Kazi yarudi kazini

Kivuko cha MV. KAZI kimerejea rasmi katika eneo la Magogoni Kigamboni kwa ajili ya kutoa huduma baada ya kukamilika kwa ukarabati wake mkubwa uliogharimu kiasi cha Tsh. Bilioni 4.4. Kivuko hicho kiliondolewa kwenye maji baada ya kufikia muda wake wa ukarabati mkubwa.

Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) umesema “Kilianza rasmi kukarabatiwa mwezi Juni mwaka 2022 na Mkandarasi Songoro Marine Transport Boatyard katika yadi yake iliyopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam.”

“Katika mpango wa maendeleo wa miaka mitano 2020-2025 na kupitia Wizara ya Ujenzi, Serikali imeanza kutekeleza ahadi hizo kwa kuanza kuvifanyia ukarabati vivuko hivyo,” aliongeza.

“Serikali inayoongozwa na Rais Dr. Samia Suluhu Hassan ilitoa ahadi mbalimbali kwa wananchi ikiwemo kuboresha huduma za vivuko hapa nchini ili kuwapunguzia wananchi kero za usafiri wanazopata katika maeneo mbalimbali kupitia Wizara mbalimbali.”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post