Mtu mchafu zaidi Duniani afariki baada ya kuoga kwa mara ya kwanza

Mtu mchafu zaidi Duniani afariki baada ya kuoga kwa mara ya kwanza

Mtu anayesadikiwa kuwa mchafu kuliko wote Duniani Amou Haji a.k.a Mjomba Haji (94), amefariki dunia nchini Iran miezi michache baada ya kuoga kwa mara ya kwanza baada ya miaka takribani 67 .

Mwaka 2014 gazeti la Tehran Times liliripoti kuwa mtu huyo alikuwa akila wanyama waliogongwa na magari barabarani, alivuta sigara ama bomba zenye kinyesi cha wanyama na aliamini kuwa usafi ungemfanya augue.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la IRNA la nchini Iran, wanakijiji wamesema kuwa mjomba Haji alikumbwa na matatizo ya kihisia ujanani na yalimpekekea kukataa kuoga na kuanza kuamini zaidi kwenye uchafu. Miezi michache iliyopita, wanakijiji walifanikiwa kumshawishi kuoga.



Baada ya kifo chake rekodi hii isiyo rasmi sasa inashikiliwa na mzee mmoja nchini India Kailash Singh maarufu kama "Kalau" ambaye mwaka 2009 aliripotiwa na gazeti la Hindustan Times akiwa hajaoga kwa Zaidi ya miaka 30.

Aidha Kalau amewahi kusema kuwa ameamua kutooga ili kuweza kuombea matatizo ya taifa la India. Kila siku ifikapo jioni hupendelea kuwasha moto,kuvuta bangi na kusimama kwa mguu mmoja akisali.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post