Kwenye picha ni hayati Mzee Mwinyi akiwa na mfalme wa muziki wa Pop Michael Jackson alipotembelea nchini Tanzania mwaka 1992.
Michael alifika Tanzania siku ya Jumatano, Februari 17, 1992, katika ziara yake akiwa kama Balozi wa Umoja wa Mataifa, alifika jijini Dar es Salaam na ndege yake binafsi akitokea Ivory Coast na kupokelewa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wakati huo, marehemu Hassan Diria.
Katika ziara yake Michael ambaye anatajwa kama msanii mkubwa duniani, alikutana na hayati Mzee Mwinyi na kisha siku iliyofuata alitembelea shule maalumu ya watoto yatima na wenye mtindio wa ubongo iliyokuwa Sinza. Ziara ya MJ Afrika pia ilihusisha kushuti kwa ajili ya video yake ya Return to Afrika.
Leave a Reply