Mfahamu mwanaume ambaye hajawahi kuona wanawake

Mfahamu mwanaume ambaye hajawahi kuona wanawake

Waswahili wanasema ukistaajabu ya Musa utaona ya firauni, kwa karne ya sasa ni ngumu, kukutana na binadamu ambaye hajawahi kuona mwanamke au mwanaume toka azaliwe kwani watu wamekuwa wakionana na kujuana kupitia njia tofauti tofauti.

Kwa mujibu wa gazeti la Edinburg Daily Courier lililotolewa Oktoba 29, 1938 lilizua taharuki baada ya kuandika historia ya mtawa wa Kigiriki ambaye anadaiwa kuishi maisha yake yote bila kuona wanawake.

Mihailo Tolotos alizaliwa mwaka 1856 mama yake alifariki saa nne baada ya kumzaa, kwakua hakuwa na baba wala ndugu wengine wasamalia wema walimchukua na kwenda kumuacha kwenye ngazi za makao ya watawa wanaume juu ya Mlima Athos uliopo Ugiriki.

Watawa walimchukua na kumpa jina la Mihailo Tolotos, akiwa ndani ya Milima hiyo aliripotiwa kuwa aliishi maisha yake yote kwa kumcha Mungu, kufunga kuomba pamoja na kufanya kazi, hakuwahi kuona filamu, ndege, wala magari.

Ndani ya majengo hayo moja ya sheria zilikuwepo kwa zaidi ya miaka elfu moja katika Mlima Athos ni wanawake hawakuruhusiwa kuingia katika eneo hilo huku sababu ya sheria hii ilikuwa kuhakikisha kwamba watawa wote wanaoishi katika monasteri zote za Mlima Athos wangeweza kutimiza takwa lao la kukaa useja kwa maisha yao yote.

Tolotos aliishi katika kuta za jengo hilo kwa furaha bila kuona tofauti yoyote ambapo kwa mujibu wa baadhi ya vyombo vya habari vilieleza kuwa alikuwa akisikia stori kuhusu wanawake lakini hajawahi kuwaona mpaka alipofariki mwaka 1938 akiwa na umri wa miaka 82 kwa kuwa hakuwahi kuona wanawake maishani mwake watawa walimpa maziko maalum.Majengo ya Athos ni makazi maalumu ya Watawa wa kiume yanayopatikana Ugiriki ambayo yanahistoria ndefu ya kuzingatia sheria kali ya kuzuia wanawake kuingia katika majengo hayo, sheria hiyo inayojulikana kama ‘Avaton’, imekuwa ikitumika kwa zaidi ya miaka elfu moja na inatokana na imani kwamba uwepo wa wanawake unaweza kuvuruga usafi wa kiroho wa Watawa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post