Kikundi cha wapelelezi 11 nchini Urusi walisafiri kwa takribani siku 36 kwa ajili ya kupeleleza kwenye baadhi ya mipaka nchini humo ambapo baada ya kumaliza kazi hiyo walilazimika kusalia katika bahari ya Antartic baada ya kukumbana na msimu wa theluji.
Tovuti ya Daily mail imeeleza kuwa miongoni mwa wapelelezi hao alikuwepo daktari wa upasuaji aitwaye Leonid Ivanovich Rogozov, mwenye umri wa miaka 27, ambaye wakati wa safari hiyo alikuwa akihisi maumivu makali ya tumbo.
Kwa mujibu wa dialy (shajara) ya Rogozov ilieleza kuwa anahisi kama anaugonjwa wa appendicitis’ (apendeksi) lakini aliamua kukaa kimya kutokana na kutokuwa na mtu anayeweza kumpatia msaada.
Aprili, 30, 1961 hali ilikuwa tete kwa upande wake ndipo akaona asingeweza kuvumili maumivu hayo na kuamua kuchukua maamuzi ya kujifanyia upasuaji mwenyewe.
Kutokana na maamuzi hayo aliamua kuwashirikisha wenzake na kuwaomba wamsaidie katika upasuaji huo ndipo akaamua kuchagua timu ya watu watakaomsaidia, ambapo aliwafundisha jinsi ya kuchoma sindano yenye dawa, jinsi ya kumpa hewa pindi atakapo karibia kupoteza fahamu, kushika taa, kumuwekea kioo ili aweze kuona anachokifanya.
Siku iliyofuata saa 2 asubuhi alijichoma sindano ya ganzi na baada ya dakika 15 kupita alianza kujifanyia upasuaji uliochukua takribani dakika 50 mpaka kukamilika.
Baada ya kumaliza aliwataka wasaidizi wake wamchome sindano ya usingizi na kusafisha vifaa walivyotumia katika upasuaji huo. Kwa mujibu wa wasaidizi wake waliweka wazi kuwa Rogozov alianza kurudi
katika hali yake siku nne baada ya kujifanyia upasuaji huku akichukua wiki mbili tuu kurudi katika majukumu yake ya siku zote.
Timu hiyo ya wapelelezi 11 ilikaa katika bahari ya Antartic kwa mwaka mmoja na kurudi katika taifa lao Mei 29, 1962 wakiwa wazima wa afya.
Rogozov alirudi kazini katika kliniki aliyokuwa akifanya kazi na aliteuliwa kufundisha Idara ya Upasuaji Mkuu wa Taasisi ya Kwanza ya Matibabu ya Leningrad kwa maisha yake yote.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply