Mchungaji awatimua waumini wenye digrii Kanisani

Mchungaji awatimua waumini wenye digrii Kanisani

Mchungaji wa Kanisa la Neno nchini Kenya, James Ng’ang’a amewaacha watu wengi midomo wazi baada ya kutoa onyo kwa waumini wake waliohitimu shahada ya kwanza kuwa waache kuhudhuria kanisani hapo endapo hawatamsikiliza mafundisho yake.

Tamko la Ng’ang’a linakuja wakati ambapo mijadala inaendelea kuhusu mapendekezo ya Serikali ya Kenya kudhibiti makanisa, na kuwataka wachungaji kuwa na elimu ya msingi ya Thiolojia.

Kwenye video iliyochapishwa mitandaoni, Ng’ang’a, anaskika akirusha maneno na matamshi mazito kuhusu washirika wake wenye shahada.

“Wenye shahada msije ninapohubiri, nendeni kwenye makanisa yenu mnayohudhuria ibada fupi za dakika mbili, hamuwezi kutawala mambo ya kiroho. Hao wasomi tuheshimiane, Daudi hakujifunza na hata manabii aliowapaka hawakujifunza,” amesema.

Ng’ang’a pia alishutumu watu waliosoma kwa kuumiza ulimwengu, haswa kuhusu masuala kama vile mapenzi ya jinsi moja.

“Watu wasomi wameharibu dunia. Hao ndio wameleta suala hili la mapenzi ya jinsi moja. Majaji waliidhinisha, na sisi sote tuliona na kushuhudia. Kisha mnasema wahubiri ambao hawajasoma hawaweziku hubiri nchini Kenya, aje? Kwa nini?” ameshagaa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BirudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post