Mbu hatari kutoka bara la Asia ahamia Afrika

Mbu hatari kutoka bara la Asia ahamia Afrika

Wanasayansi wanasema kwamba aina vamizi ya mbu anayeeneza malaria kutoka Asia imeenea hadi Afrika, ambako ni tishio hasa kwa wakazi wa mji huo.

Mbu huyo tayari amesababisha visa vya ugonjwa huo kuongezeka nchini Djibouti na Ethiopia, na hivyo kutatiza juhudi za kutokomeza ugonjwa huo.

Watafiti wanasema iwapo aina hii ya mbu “Anopheles Stephensi”atasambaa kwa wingi barani Afrika anaweza kuwaweka karibu watu milioni 130 hatarini.

Mtafiti aliyebobea katika uchunguzi wa aina hiyo ya mbu Sarah Zohdy anasema“Ushahidi upo unaoitaka Dunia kufanyia kazi tatizo hili”.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post