Mbinu za kuuza na kupata oda katika biashara yako

Mbinu za kuuza na kupata oda katika biashara yako

Niaje niaje wafuatiliaji wa Mwananchi Scoop, haya sasa tuendelee tulipo ishia, all in all week iliopita bwana tumefanya biashara haswa tusifichee, wenye kuuza nguo, vyakula, vinywaji nk hii sikukuu ama kweli haijatuacha vibaya tuseme tuu ule ukweli.

Sasa leo katika segment yetu ya biashara bwana tumekusogezea mada moja matata sana ambayo ukiisoma na kuielewa vizuri itakusaidia san asana katika biashara yako.

Wafanyabiashara wengi wanatamani sana kukuza, kuuza na kupata oda katika biashara kama wanavyofanya wauzaji wa kubwa mfano Esma dangote, lakini hawajui ninifanyanye ili waweze kukuza biashara zao. Kwa ufupi sana leo tunawajuza kuhusiana na mbinu za kuuza na kupata oda katika biashara yako.

Ikiwa umeamua kutumia jukwaa la mitandao ya kijamii kuitangaza biashara yako lazima uwe mbunifu. Kwanza kabla hatujaelekezana mbinu za kuuza na kupata oda inabidi tutambue aina mbalimbali za jumbe ambazo zinaweza kuwa na athari chanya kwa wateja wako na kuwafanya wafanye kitendo kama vile kuweka oda, kutoa like, na kuacha maoni kwenye ukurasa wako wa biashara.


Hizi ni baadhi ya aina hizo za ujumbe au kwa kingeleza tunaita (Caption) zinazoweza kukufaanya ukauza na kupata oda katika biashara yako

Caption zitakazokusaidia kutatua tatizo.
Ujumbe (caption) ambazo zinawasaidia wateja wako kutatua tatizo fulani ambalo wanakabiliwa nalo unaweza kuwa na faida kubwa katika biashara yako.

Wacha nikutolee mfano sisi wateja siku zote huwa tunapenda sana kuuliza maswali so ili wewe kuepuka maswali hayo katika post ya bidhaa yako inabidi utoe maelezo yote kuhusiana na bidhaa hiyo ili mtu yoyote akifanikiwa kuiona basi asiwe na swali hata moja yaani akute full package.

Caption zinazowasilisha faida
Ikiwa unataka wateja wako waweze kununua bidhaa yako ni muhimu
kuwaelezea faida ambazo watapata kwa kutumia bidhaa hiyo. Mfano mkubwa kwa wale wanofanya biashara za mafuta, scrub na sabuni.

Ni vyema ukatoa maelekezo na faida watakazo zipata katika bidhaa yako hii pia itamfanya mteja atakae kuja awe na mashaka na biashara yako.

Caption za punguzo la bei
Hahahahha!  Make hapa kwanza ncheke hivi mnajua kuwa hii ndio secta ambayo wateja wengi wanaipenda yaani nakwambia kwa herufi kubwaq wateja wengi wanavutiwa na punguzo la bei, ofa au matangazo mengine.

Kwa hivyo unaweza kuwatumia ujumbe wa aina hii ili kuwafanya wawe na nia ya kununua bidhaa yako.

Kutoa ujumbe unaotoa habari mpya


Wakati mwingine kutoa habari mpya kuhusu bidhaa yako au kutoa habari muhimu kwa wateja wako kunaweza kuwasaidia kuwa na nia ya kuchukua hatua ya kufanya biashara nawewe.

Chakufanya kila ukiwa na bidhaa mpya nenda katika mitandao yako ya kijamii yote wajuze hii itakuwa inamsaidia mteja kujua bidhaa mpya na yazamani ili asiweze kutapeliwa huko kwingine, fanya kurasa zako kuwa special kwa wateja wako.
Na hizi hapa ndio mbinu zitakazo kusaidia kusaidia kuuza, kukuza na kupata oda katika biashara yako…

  • KUTOA HUDUMA BORA

Cha kwanza ili biashara yako iweze kukuua na kupata oda kwa wingi kama wafanyabiashara wakubwa humo mitandaoni ni kuwa na huduma bora kwa wateja wako, na kama ilivyo ada ukitoa huduma bora kwa mteja mmoja tuu basi huyo huyo ndio ataenda kufikisha habari kwa wateja wengine.

Tunajua kama biashara ni wito so jitahidi hata kuweka vigift katika bidhaa zako ili uweze kuwavutia wateja wako waweke oda kabla hata bidhaa kufika.

  • KUFANYA PROMOSHENI

Ili biashara yako iweze kukua, kuuza Zaidi na watu waweze kuweka oda kwa wingi ni kufanya promosheni ya bidhaa zako, hii sasa unaweza kuitumia kwa zile bidhaa ambazo umezinunua muda mrefu na hazikuuzika yaani zile za zamani ili uweze kuingiza mzigo mpya.

Unaweza kufanya hivyo kwa kupunguza bei ya bidhaa au kuudha bidhaa mbili, tatu kwa bei ya chini, hii itakusaidia watu wengi waweze kuweka oda na kuuza kuliko hata unavyofikiria. Mfano mkubwa angalia anachokifanya Freddy Vunjabei ndo utaelewa nini namaanisha.

  • KUULIZA MAONI

Kama nilivyosema hapo awali wateja wengi wanapenda sana kujiskia wako nyumbani yaani anahitaji umpokee kwa ukarimu umuhudumie kwa ukarimu yaani wewe hata kama umeandika bei lakini akauliza kwenye comment wewe mjibu tuu.

Wateja kutoa maoni juu ya bidhaa au huduma zinazowahamasisha wateja wako hii italeta ukaribu wa kuwasiliana kibiashara na wateja pia kukuongezea kujenga uaminifu wa wateja na biashara.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post