Mavazi ya kuepuka endapo una kimo kidogo

Mavazi ya kuepuka endapo una kimo kidogo

Ebwanaa mambo niaje? Karibu sana kwenye ulimwengu wa fashion mdau wangu, sehemu yetu pendwa kabisa ya kujidai na kuhakikisha tunaweka sawa mionekano yetu mbele ya kadamnasi bwana.

Nikwambie tu kuwa wiki hii tutaangazia mavazi ya kuyaepuka endapo utajigundua kuwa una mwili au kimo kidogo, unaionajee hii mtu wangu?

Nikufahamishe kuwa kupata mavazi ambayo yanaendana na kimo chako inaweza kuwa ni tatizo ambalo unakutana nalo mara kwa mara endapo wewe ni mfupi, yes hii inakuwa kama zamani ambapo watu wanene walikuwa wakikosa mavazi kutokana na makampuni kutumia sana vipimo vya models wembamba same na kwa wafupi makampuni mengi hutumia vipimo vya models warefu, ukipata mavazi basi lazima upeleke kwa fundi yapunguzwe.

Well, leo tunaongelea vitu vya kuepuka endapo una mwili mdogo (mfupi).

  • Oversized Clothing

Tayari una mwili mdogo usiufunike zaidi kwa kuvaa mavazi makubwa. Yes, ni shida kupata mavazi yanayotutosha lakini mafundi wapo. Hakikisha fundi ni rafiki yako, vaa mavazi yanayokutosha vyema na kama utavaa moja oversized basi lingine liwe perfect fit usivae juu na chini kote oversize.

  • Low Rise Jeans

Wengi tunapendelea kuvaa hizi ukizingatia wengi wenye maumbo haya huwaga hawana matumbo inakuwa perfect way ya kushow off, lakini tunasahau kwamba hizi suruali zinafanya kuonekena mfupi zaidi, badala yake vaa highwaist ambayo itakufanya miguu yako ionekane mirefu kuliko ambavyo ipo. 

  • Chunky Shoes

Inawezekana katika fikra unawaza hivi viatu vinasaidia kuleta urefu lakini kiukweli hivi vinakumeza na vinatoa attention yote kwako na kupeleka miguuni na vinafanya uzidi kuonekana mdogomdogo. Badala yake chagua viatu ambavyo simple havina mambo mengi kama converse, oxfords au kama ni mpenzi wa heels basi vaa heels zisikukuwa chunky au platform.

  • Oversized Handbag

Oversized handbags ni sawa na chunky shoes, zinakumeza unazidi kuonekana mdogo, badala yake chagua medium size ambazo zinaendana na mwili wako na kufanya attention isiondoke kwako.


Ni matumaini yangu umejifunza jambo. tuambie unapata shida gani katika mavazi? Funguka mtu wangu ili tujue tunatatua vipi changamoto hiyo have a nice weekend na tutashare hapa namna ya kutatua shida hio.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post