Kampuni ya DELL kuwaachisha kazi wafanyakazi 6,650

Kampuni ya DELL kuwaachisha kazi wafanyakazi 6,650

Kampuni ya kuunda vifaa vya kielektroni ya DELL itawaachisha kazi wafanyakazi 6,650 sawa na 5% ya wafanyakazi wote kutokana na mauzo ya kompyuta kupungua kwa 28% kila mwaka.

DELL iliripoti kushuka kwa soko lake la nje la kompyuta zake kwa 37% katika kipindi cha mwaka 2022 huku washindani wao, kampuni za Lenovo zikishuka kwa 28%, HP  29% na Apple  2%.

Aidha kufikia Januari 28, 2023, DELL ilikuwa na Wafanyakazi 133,000.

Kampuni nyingine za teknolojia zilizopunguza wafanyakazi hadi sasa ni PayPal, Twitter, Google, Microsoft, Salesforce, Amazon, META , Adobe, Cisco , HP na Intel.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post