Jinsi ya kukabiliana na stress za kazi

Jinsi ya kukabiliana na stress za kazi

Msongo wa mawazo ni hali ya shinikizo la kiakili au la kihisia linalotokana na mahitaji yanayofikiriwa. Kila siku, tunakabiliwa na hali nyingi ngumu ambazo wakati mwingine tunaziona kama vitisho (kwa mfano, mzigo mkubwa wa kazi na kutunza familia zetu).

Moja ya jambo ambalo limekuwa jipu kwa baadhi ya wafanyakazi ni kukutana na stress za kazi, na kutoelewa njia za kuepukana na hilo.
Kutokana na hilo Mwananchi Scoop imekusogezea njia kadhaaa zitakazoweza kukusaida kuondokana na msongo wa mawazo uwapo kazini.

Pangilia kazi zako
Stress za kazi humfanya muhusia aishi maisha ya hofu muda wote na kufanya apunguze ubunifu eneo la kazi. Ili kupunguza au kuondokana na stress kazini unatakiwa kupangilia ratiba zako vizuri.
Mfano ukiwa unatoka kazini Jumatatu hakikisha unajua Jumanne utakuwa na majukumu gani na lipi utaanza kulifanyia utekelezaji, hii itakusaidia.


Kubali changamoto
Katika maisha kila binadamu anakumbana na changamoto mbalimbali hivyo ili kuepusha msongo wa mawazo kazini unatakiwa kukabiliana na changamoto unazokutana nazo na siyo kuzikwepa either ziwe za binafsi au za ofisini unachotakiwa ni kukabiliana na kila kitu.

Sometimes stress za kazi zinaweza kuchangiwa na boss wako au mazingira ya kazi unachotakiwa kufanya ni kujua njia sahihi ya kupambana na suala hilo, jambo la msingi la kuzingatia ni kuweka mbali stress za kazi na mambo binafsi.

Epuka mikwaruzano na boss wako
Baadhi ya stress zinaepukika kama hii ya kugombana na boss wako, wapo baadhi ya ma-boss ambao wakitibuliwa katika familia zao hasira wanamalizia kwa wafanyakazi ili na wewe asikuingize katika hasira zake muepuke na deal na mambo yako yaliokupeleka kazini.

Nimezungumzia suala hili kwa sababu wapo baadhi ya watu wanaoamini kuwa stress zinaletwa tu na kazi lakini bila kujua kuwa hadi waajiri wanaweza kusababisha ukose amani.


Jifunze kusema hapana
Unajua kwenye kila ofisi kuna tabia ya kupeana vikazi visivyoeleweka hata vimetokea wapi, unaposema hapana inakuondolea stress za kuwa na kazi mbili mbili.

Ukijifunza kusema hapana na wala siyo ile ya kukataa kabasa mueleweshe vizuri kuwa una kazi unafanya ili kuepusha stress ndogo ndogo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post