Je wajua Wanaume wenye vipara walitumika katika majaribio ya lipstick

Je wajua Wanaume wenye vipara walitumika katika majaribio ya lipstick

Katika miaka ya 1950 kazi ambayo ilikuwa ikitrend sana katika sehemu mbalimbali hasa Marekani ni kazi ya majaribio ya lipstick iitwayo ‘Lipstick Tester’ ambapo kampuni za utengenezaji urembo huo zilikuwa zikitoa donge nono (mshahara) kwa wanaume wenye vipara kwa ajili ya kupigwa mabusu maeneo mbalimbali ikiwamo kichwani kwa lengo la kujaribu bidhaa hiyo ya urembo.

Kazi hiyo ambayo ilikuwa ikimtaka mwanaume kuingia kazini kila siku kwa ajiri ya kupigwa mabusu na akina dada ambao wafanyakazi wa kampuni hiyo ikiwa kama majaribio ya lipstick ambazo zimetengenezwa kwa siku hiyo.

Majaribia hayo yalikwisha baada ya baadhi ya watu kulalamika kuwa kazi hiyo ni udhalilishaji kutokana na wengine kuwa ni waume za watu, hapo ndipo mshauri wa vipondozi Rae Morris, alitoa njia mbadala za kujalibu urembo huo.

Ambapo alieleza kuwa wanaotumia mikono kama majaribio ya vipodozi hivyo wanakosea kwani ngozi ya mkono na lipsi ni vitu tofauti hivyo anashauri watu kutumia kidole kuangalia lipstick kama inamfaa kuitumia.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post