Irani yaongoza hukumu ya kunyonga

Irani yaongoza hukumu ya kunyonga

Shirika moja la kutetea haki za binadamu lilisema Jumatatu nchi ya Iran imewanyonga watu wasiopungua 354 katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu na kuongeza kuwa kasi ya kuwanyonga watu ilikuwa kubwa zaidi kuliko mwaka 2022.

Shirika hilo lenye makao yake makuu nchini Norway lilisema, idadi hiyo ya watu 354, kwa miezi sita ya kwanza, hadi Juni 30, ilikuwa asilimia 36 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2022, ambapo watu 261 waliuawa.

Aidha ikisisitiza wasiwasi kwamba makabila yasiyo ya uajemi yameathiriwa kupita kiasi kutokana na kunyongwa kwa watu nchini humo.

Huku watu 206 walinyongwa kwa mashtaka yanayohusiana na dawa za kulevya, ambalo ni ongezeko la asilimia 126, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Wanawake sita walikuwa miongoni mwa walionyongwa katika kipindi hicho, huku wanaume wawili wakinyongwa hadharani, ilieleza ripoti hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post