Rudeboy: Hakutakuwana kundi la Psquare tena

Rudeboy: Hakutakuwana kundi la Psquare tena

Mwanamuziki kutoka Nigeria Paul Okoye maarufu Rudeboy amethibitisha kuwa kundi la ‘Psquare’ alilolianzisha yeye na pacha wake Peter Okoye limevunjika milele.

Rude ameyasema hayo wakati alipokuwa live Instagram baada ya mashabiki kumuuliza kuhusu hatima ya kundi hilo ndipo akaweka kazi kuwa hayupo tayari kuungana tena na kaka yake Peter huku akizungumza kwa mafumbo na kudai ‘siku za kula pesa huku nyani anafanya kazi zimeisha’.

“Rude wa sasa ni mpya, eh, zile siku ambazo nyani anafanya kazi na baboon anakula, sitafanya hivyo tena. Nimeamua kufanya kazi kwa ajili yangu mwenyewe. Nilikuwa daima ndiye ninayetunga nyimbo zote, sitafanya hivyo tena na hatuwezi kuungana milele.”

Ikumbukwe kuwa mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka huu Paul Nonso Okoye ‘Rudeboy’ alithibitisha kusambaratika kwa kundi la PSquare kwa mara nyingine kwa kudai kuwa toka walivyoungana hakuna cha maana kilichowahi kufanyika.

Kundi la P-Square lilisambaratika kwa mara ya kwanza mwaka 2016 na kuungana tena mwaka 2021, huku mwishoni mwa mwaka jana kukiwa na tetesi kuwa wawili hao wamegawanyika tena.

Wawili hao walitamba na ngoma zao kama ‘Taste The Money (Testimony )’, ‘Personally’, ‘Forever’ pia wamewahi kutoa kolabo na mwanamuziki Diamond wimbo uitwao ‘Kidogo’






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags