Aliyejitoa Zabron Singers afunguka

Aliyejitoa Zabron Singers afunguka

Baada ya kuzuka minong’ono kupitia mitandao ya kijamii ikidai kuwa aliyekuwa mwanamuziki wa kundi maarufu la nyimbo za Injili, Jamila Dotto kuwa ameondoka katika kundi kwa ugomvi, hatimaye msanii huyo amekanusha tuhuma hizo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Jamila amefunguka kuwa aliondoka katika kundi la ‘Zabron Singers’ kwa wema na siyo kama watu wanavyozungumzia.

“Naitwa Jamila Dotto nipo hapa kukanusha taarifa ambazo zinasambaa mitandaoni kuhusiana na mimi kuondoka katika kundi la ‘Zabron Singers’, mimi niliondoka kwenye kundi hilo kwa wema na tulikaa kikao na viongozi wa kwaya ya Zabron nikaondoka kwa wema, nikawaaga na wakaniruhusu.

"Kwa sababu mimi nilichukuliwa kujiunga na kundi la ‘Zabron Singers’ ilikuwa ni kwa ajili ya kukuza kipaji changu lakini pia kufanya injili pamoja, kwa hiyo chochote kinacho zungumzwa kuhusu mimi au ‘Zabron Singers’ siyo cha kweli na hata kama kuna ukweli siyo kama vile unavyoelezewa kwenye mitandao ya kijamii.” amesema Jamila

Mbali na hayo amefunguka kuwa yeye hana ugomvi na mtu yoyote katika kundi hilo kwani amekuwa akiomba ushauri kuhusu kazi zake na wamekuwa wakimsaidia kadri wawezavyo.

Jamila akiwa ndani ya ‘Zabron Singers’ sauti yake imesikika kwenye nyimbo kama ‘Sweetie Sweetie’, ‘Usiniache’, ‘Nawapenda’ nk, hata hivyo baada ya kujitoa katika kundi hilo ameshaachia nyimbo kama ‘Umenisaidia’, ‘Fungua Njia’ akimshirikisha Japhet Zabron, ‘Asante kwa wema’, ‘Ninakuamini’ na ‘Rafiki Yangu’.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags