Fahamu Vidonda vya Tumbo na dalili zake

Fahamu Vidonda vya Tumbo na dalili zake

Ugonjwa wa vidonda vya tumbo ni moja ya magonjwa ambayo yamekuwa yakiathiri afya ya binadamu wengi hapa nchini na duniani kwa ujumla.

Kwa wakati tulio nao, hili ni tatizo la kawaida maana limewapata watu wengi na halisababishi vifo vya watu wengi kama maradhi ya saratani na kisukari.

Rahel Mwinuka ni Daktari wa magonjwa ya binadamu kutoka Hospitali ya Anglikana, iliyopo Buguruni jijini Dar es Salaam na anafunguka na kusema vidonda vya tumbo husababishwa na mmengenyo wa chakula kushindwa kufanya kazi vizuri.

Alisema vidonda hivyo pia utokana na mashambulizi ya bakteria wanaoitwa Helicobacter pylori (Hpylori) au kulika kwa ukuta wa tumbo kutokanana na athari za tindikali zilizopo tumboni (stomach acids) kama vile tindikali ya hydrocloric yaani hydrocloric acid.

“Vidonda hivi vimegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Gastric ulcers ambapo hivi hutokea ndani ya tumbo la chakula na duodenal hivi hutokea kwenye sehemu ya juu ya utumbo mdogo inayoitwa duodenum,” alisema na kuongeza

“Hao ni wagonjwa waili tofauti wa vidonda vya tumbo lakini dalili zake uwa zinafanana na kutofautiana kidogo kwani yupo ambaye akila chakula anasikia maumivu na huyu mwingine akila chakula nakaa muda na ndipo usikia maumicu,” alisema

Dalili za ugonjwa huo

Dk. Mwinuka alisema moja ya dalili ya vidonda vya tumbo ni umbo kujaa gesi, kupata choo cha mbuzi, kiungulia, maumivu ya tumbo kutokea kitomvuni mpaka kifuani, kukosa hamu ya kula, kupungua uzito bila sababu na kuchoka sana.

“Dalili ya kawaida ya vidonda vya tumbo ni maumivu ya tumbo. Asidi ya tumbo hufanya maumivu kuwa mabaya, kama vile kuwa na tumbo tupu yaani ukiwa na njaa,”

Anasema dalili mbaya ya vidonda hivyo ni mtu kupata choo cheusi ambacho uashiria kuna mahali damu inavujia.

“Ipo pia dalili za kutapika damu, kusikia kichwa kinauma, mwili kuchoka, kukosa hamu ya kula, ikumbukwe hizi ni dalili kwa mtu ambaye tayari ameanza kupata ugonjwa huo,” alisema

Maumivu yanaweza kupunguzwa kwa kula vyakula fulani ambavyo hupunguza asidi ya tumbo au kwa kutumia dawa ya kupunguza asidi, lakini kisha inaweza kurudi. Maumivu yanaweza kuwa mabaya kati ya milo na mlo na wakati wa usiku.

Vidonda vya tumbo vinatibika

Anasema licha ya kwamba vidonda hivyo vinatibika watu wamekuwa wakifika hospitalini wakiwa wana zaidi ya miezi miwili tangu waugue ugonjwa huo.

“Life staily yetu inatuumiza unakuwa unampatia mgonjwa vigoje vya kumewza lakini akijiona,amepona uvitupa vidonge hivyo kabla ya kuma wa dozi kumalizika,” anasema

Hata hivyo alisema wamekuwa wakitoa masharti kwa wagonjwa wa vidonda hivyo kwa kuwataka kuacha kula vyakula vya aina mbalimbali lakini wengi wao wamekuwa wakigoma kuyafuata maelekezo yanaytolewa na wataalamu wa afya.

Namna ya kuishi na vidonda vya tumbo

Alisema ili kuweza kuishi na ugonjwa huo unapaswa kula lishe yenye afya yaani ile iliyojaa matunda, haswa ya vitamini A na C, mboga mboga, na nafaka nzima.

“Kutokula vyakula vyenye vitamini vingi kunaweza kuifanya iwe ngumu kwa mwili wako kuponya kidonda chako,” alisema Dk.

Pia alisisitiza kuwa mtu mgonjwa anapaswa kudhibiti msongo wa mawazo ili hasiweze kuzidisha ishara na dalili za kidonda cha tumbo.

Lakini pa Dk. Mwinuka amewataka wanaume kuacha uvutaji wa sigara kwani  unaweza kuharibu utando laini unaolinda tumbo na kulifanya  liweze kuhusika na ukuaji wa kidonda.

Vitu vya kufanya usipate ugonjwa huo…

Dk. Mwinuka anasema ili mtu asiweze kupata vidonda vya tumbo anapaswa kutokaa muda mrefu bila kula.

“Kuna watu wanakula mara tatu lakini ile ya kuchelewa sana unakuta mtu anakunywa chai saa nne, chakula cha mchana saa 10 jioni na cha usiku ni saa nne au tano, huyo mtu tayari yupo katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo.

Alisema watu hao wapo katika hatari hiyo kwa sabbau ukaa muda mrefu bila kula hivyo kusababisha tumbo kuwa tupu muda mrefu na acid zinazoshuka ukutana na utupu huo.

Anasema vyakula ambavyo vinaweza kusabbaisha vidonda ni vile vyenye gesi na acid kwa wingi hivyo amewataka watu kuacha kuvitumia mara kwa mara ili kujiondoa katik liski ya kupata magonjwa hayo.

“Unakuta mtu anakula lakini amejaza pilipili nyingi ambapo akila anaisikia jinsi inavyoingia tumboni, hapa nieleweke sikatazi watu kula pilipili bali wale kwa kiasi kwani ikizidi inamadhara,” alisema

Aidha aliishauri jamii pindi inapopata magonjwa ya tupo inapaswa kwenda hospitali kupata vipimo ikiwemo choo kikubwa ili kujua nini kinaendelea kwenye mfumo wake wa mmengenyo wa chakula.

Aidha Dk. Mwinuka amewataka wale ambao wanaugua vidonda hivyo kutumia dawa kama inavyotakiwa ili waweze kupona na taifa iondoe ugonjwa huu.

“Vidonda hivi vya tumbo vimekuwa vinafananisha na magonjwa mengine unakuta mtu anaumwa chembe ya moyo anasema vidonda,” alisema na kuongeza

“Tunatakiwa kuwafanyia concelling wale wote wanaougua ugonjwa huu kwani ukifuata masharti unapona kabisa,”

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post