Fahamu Madhara ya kiafya, kuwa na wapenzi wengi

Fahamu Madhara ya kiafya, kuwa na wapenzi wengi

Ni Alhamisi nyingine tena, yenye utulivu na usikivu kwa wasomaji wangu wa nguvu kabisa. Naamini wengi wenu mpo salama kabisa hapo chuoni na mmekaa mkao wa kupokea nilichowaandalia leo.

Basi leo katika Makala ya afya tumekutana na mshauri wa vijana na mwanasaikolojia Dk. Elizabeth Lema ambaye amefunguka juu ya madhara ya kiafya anayoweza kuyapata mtu mwenye kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi na wapenzi wengi.

Akizungumza na MwananchiScoop, Dk. Lema anasema kuwa katika ulimwengu wa sasa vijana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na zaidi ya mtu mmoja ni kitu cha kawaida kwao.

Hata hivyo Dk. Lema anasema kusheheni wapenzi kuna madhara mengi ambayo mtu anaweza kuyapata ambapo madhara hayo ni kuwa katika hatari ya kupata magonjwa ya zinaa na Ukimwi na hatimaye kupelekea kifo.

Anasema vijana wengi wanapofikia umri wa kupevuka wanakuwa na nguvu fulani wanayodhani inaweza kuwepo daima hivyo ujikuta wanajiingiza katika suala la kuwa na mahusiano ya kimapenzi na watu wengi na kusahau jambo hilo linaweza kuwasababishia maradhi.

“Mimi naumia sana na wasichana waliopo chuoni unakutana anakuwa na wanaume wengi kwa lengo la kupata fedha ya kununua nguo nzuri, wigi au kutaka kutembelea gari za kifahari.

“Nakwambia wewe kijana acha kabisa hiyo tabia kwani unaweza kuangukia katika kupata magonjwa ambayo yanaweza kukatisha safari yako ya masomo hapo baadae, lakini tambua kuwa maisha ni safari unapopitia kipindi kigumu hiyo ni sehemu ya somo na uvumilivu wako ndio utakaokuja kukupatia mafanikio mbeleni,” aasema

Kuathirika kisaikolojia

Dk. Lema anasema kitu ambacho wengi hawakifahamu ni kwamba, kumiliki wapenzi wengi husababisha matatizo ya kisaikolojia, hiyo ni kutokana na wahusika kukiuka hitaji la moyo la kuwa na mpenzi mmoja ambaye atamuamini na kuwa na lengo naye moja.

“Jamani hapa nilipo napokea kesi nyingi sana unakuta kijana mwenye wapenzi wengi amefikia umri wa kuoa anaoa mwanamke lakini anashindwa kutulia naye, namsikiliza na kugundua matatizo yao siyo suala ya kimwili bali ameshaathirika kisaikolojia.

“Maana hapo anashindwa kutosheka kihisia kwani hata kama yupo tayari na mke wake faragha bado anaonekana kutamani kuwa na wapenzi wapya,” anasema

Anasema tatizo jingine la kisaikolojia la wanaojihusisha na wapenzi wengi ni ukosefu wa hamu ya tendo la ndoa wanapokuwa na wapenzi wao kwa muda mrefu kwa kuwa akili yao huzoea kuwa na wapenzi wapya ambao huwasisimua zaidi kuliko wa zamani ambao huwafanya wakinai polepole.

“Kwa hiyo kama wewe unajijua huwezi kuwa na mpenzi mmoja mpaka uwe na mwingine na kuzidi kutafuta mwingine, ujue umeshaathirika kisaikolojia.

“Cha kufanya ni kujifunga kwa dhati huku moyo wako ukijua ni ugonjwa na tiba yake ni kuachana na wapenzi wengi, baada ya muda utazoea,” anasema

Madhara mengine

Dk. Lema anasema wanaojihusisha na wapenzi wengi hasa kwa upande wa wavulana waliopo shuleni wapo katika hatari ya kupoteza nguvu za kiume na kukosa uzao.

“Tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume lipo sana kwa sasa, nikwambie tu kijana hasa wewe mwanaume, kama Mungu alikupa mayai mazuri mawili na wewe tayari ulishayatawanya huko kwa wanawake zaidi ya 10 ukija kuoa unaweza kujikuta unashindwa kupata mtoto utamlaumu nani,” anasema Dk. Lema

Dk. Lema anasema kuwa vijana wanapaswa kujua anapoanza uhusiano na mwanaume au mwanamke na kufanya naye sex wanashare damu na hisia zao.

“Sasa uwezi kuwa unagawanya vitu hivyo kwa watu wengi lazima utapata tu matatizo, nikushauri kama utaachana na uliyenaye unahitaji kujipa muda wa kutosha ili uweze kubadirika na kuzibadirisha hisia zako ndipo uanzishe mahusiano mengine,” anasema na kuongeza

“Mwili wako ukiutumia vibaya unachakaa na ukiutunza unadumu, kuna watu wanamiaka 40 ukichukua watu 10 wenye umri huo ukawaweka pamoja utaona wapo ambao wanaonekana vijana na wengine wazee

“Matokeo ya hayo yanakuwa ni kelelezo tosha wakati walivyokuwa kijana waliutumiaje miili yao na ndio maana sasa hivi unasikia life expectancy ni miaka 40 hadi 45 sio kwa sababu kwamba kuna magonjwa mengi hapana ni kwa sababu tunavyoitumia miili yetu,” anasema Dk. Lema

Ushauri

Anasema vijana wengi wa vyuo vikuu wamekuwa wakiwavunja moyo wazazi wao ambao wameangaika kuuza vitumbua ili mradi mtoto wake aende shule lakini anaishia katika kuuza mwili wake kwa kisingizo za kutafuta fedha.

Dk. Lema anasema vanawashauri vijana waliopo chuoni kuacha hiyo tabia bali wasome kwa bidii kwani bahati hiyo waliyoipata wengi waliitamani lakini hawakuweza kuipata.

“Binti ambaye unatoka na mwanaume zaidi ya mmoja kwa sababu umekosa boom, unahitaji kula vizuri au kuvaa nguo za gharama nakuomba uache mara moja, soma maisha mazuri utayakuta mbeleni,” anasema






Comments 2


  • Awesome Image
    Malichelo

    Nashuru kwa kutuletea elimu hii, pia nashauri vijana wa chuo kutumia fursa ya usomi walonao kutatua changamoto ili waweze kujipatia kipato

  • Awesome Image
    Malichelo

    Nashuru kwa kutuletea elimu hii, pia nashauri vijana wa chuo kutumia fursa ya usomi walonao kutatua changamoto ili waweze kujipatia kipato

Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post