Baada ya kuandamwa na kesi takribani nane kuhusiana na unyanyasaji wa kingono, mkali wa Hip-hop wa Marekani Diddy ameripotiwa kufanyiwa uchunguzi na familia ya Marehemu Tupac.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari mbalimbali nchini humo vimeeleza kuwa familia ya marehemu Tupac imeajiri wanasheria nguli akiwemo Alex Spiro na Christopher Clore kufuatilia madai ya Diddy kuhusika na kifo cha Tupac huku wakiamini kuwa huenda mkali huyo anafahamu kitu kuhusu kifo hicho hivyo wanataka suala hilo lichunguzwe kwa kina.
Aidha imeripotiwa kuwa Diddy alimlipa takribani dola milioni 1 sawa na Sh 2 bilioni mtuhumiwa namba moja ambaye kwa sasa yupo gerezani Keef D kukamilisha mauaji ya ‘rapa’ huyo.
Madai hayo ya Combs kuhusika na kifo cha Pac yaliibuliwa mwishoni mwa wiki iliyopita wakati Keefe D akiwa mahakamani kwa kudai yeye na wafanyakazi wenzake walilipwa fedha kukamilisha mauaji ya Tupac katika miaka ya 90s.
Utakumbuka kuwa Tupac Shakur alifariki Septemba 7,1996, baada ya kupigwa risasi akiwa kwenye gari huko Las Vegas, Nevada, huku kesi ya mauaji yake ikiendelea kulindima Mahakamani kwa zaidi ya miaka 20.
Leave a Reply