Diamond kutoana jasho na mastaa wa Nigeria, tuzo za AEAUSA

Diamond kutoana jasho na mastaa wa Nigeria, tuzo za AEAUSA

Mwanamuziki anayetamba na wimbo ‘Komasava’ Diamondplatnumz anachuana na mastaa kutoka Nigeria katika tuzo za African Entertainment Awards USA (AEAUSA) zinazotarajiwa kutolewa Novemba mwaka huu.

Hayo ni baada ya AEAUSA kutoa orodha ya wasanii na vingengele watakavyowania katika tuzo hizo, ambapo katika kipengele cha ‘Artist of the Year’ Diamond atatoana jasho na mastaa kama Burna Boy, Davido, Yemi, Ayra, Asake, Rema, Wizkid, Adekunle na msanii kutoka Afrika Kusini, Tyla.

Mbali na kutajwa katika kipengele hicho Diamond pia yupo kwenye kipengele cha ‘Best Male Artist’ akichuana na wasanii kama Davido, Harmonize, Burna Boy, Wizkid, Olamide, Rema, Kizz Daniel, Black sheriff na Fally Ipupa.

Hata hivyo, kwa upande wa mastaa wa kike kutoka Bongo Nandy ametajwa kuwania katika kipengele cha ‘Best Female Artist’ akishindana na wasanii kama Yemi Alade, Tiwa Savage, Simi, Ayra, Tems, Makhadzi, Tyla, Nandy, Aya Nakamuru na Niniola.

Aidha msanii Rayvanny kupitia wimbo wake wa ‘Sensema’ aliyomshirikisha Harmonize amechaguliwa kuwania tuzo katika kipengele cha ‘Best Collaboration’ ambapo wanaoshindanishwa ni Chris Brown ft Davido ‘Hmmm’, Tyla, Gunna Skillbeng ‘Jump’ na wengineo.

Tuzo za AEAUSA zilianza kutolewa mwaka 2015, mwaka huu zitafanyika siku mbili katika jimbo la New Jersey nchini Marekani Novemba 8 na 9.

Tuzo hizi huadhimisha na kuwaenzi watendaji katika sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na burudani, ujasiriamali na uongozi wa jamii.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post