Bilionea Elon Musk akamilisha ununuzi wa Twitter kwa bilioni 44

Bilionea Elon Musk akamilisha ununuzi wa Twitter kwa bilioni 44

Mfanyabiashara bilionea wa Elon Musk anaripotiwa kuchukua udhibiti wa mtandao wa Twitter. Awali kampuni yenye umuliki wa mtandao huo ilikataa kiwango cha dola bilioni 44 kilichotolewa na tajiri huyo lakini baade ilitangaza kumshtaki, pale alipotangaza mipamngo yake ya kuachana na biashara hiyo.

Taarifa za Alhamis za vyombo vya habari vya Marekani zilisema Elon Musk anamiliki Twitter na kwamba amewafukuza kazi watendaji wakuu wa mtandao huo. Mtendaji mkuu wa Twitter Pareg Agrawal ni miongoni mwa waliondolewa kazini pamoja na mkuu wa idara ya fedha, idara ya sheria na sera.

Musk mwenyewe amechapisha video yake katika ukurasa wake wa Twitter akionekana anatembea katika ofisi za makao makuu ya kampuni hiyo. Hata hivyo tajiri huyo na maafisa wengine wakuu wa kampuni hiyo hawajaweza kupatikana kujibu lolote kufuatia hatua hiyo.

Watumiaji wengi wa mtandao wa Twitter wameonesha wasiwasi wao juu ya ahadi ya Musk ya kulinda uhuru wa kujieleza katika jukwaa hilo iikiwa pamoja na kumrejesha rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, ambae alizuiwa katika mtandao huo kutokana na kuhusishwa na vurugu za Januari 6 katika sehemu ya Ikulu ya Marekani mjini Washington.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post