Atham: kazi yangu pambano langu la kwanza

Atham: kazi yangu pambano langu la kwanza

Ebwana eeeh!!! kila moja kwenye haya maisha huwa anamipango yake na anagombania goli kupitia malengo aliyojiwekea kichwani mwake katika safari nzima ya kutengeneza maisha yake.

Iko hivyo bwana ukatae ukubali lakini hiyo ndiyo hali halisi na namna mambo yanavyokwenda kwa vijana wengi ambao wanamalengo makubwa ya kufika mbali kupitia kazi au shughuli ambazo wanazifanya.

Abdulhamid Thabit Mzee maarufu kama Atham ni mwanafunzi kutoka Chuo cha Zanzibar University (ZU) akiwa anachukua course ya Business Information Technology yaani (BIT) akiwa  mwaka wa kwanza chuoni hapo.

Akizungumza na Mwandishi wa makala haya, Atham anasema kuwa yeye ni kijana na nimwanaharakati wa masuala mbalimbali lakini kazi yake ndiyo pambano lake la kwanza.

“Ninachokiamini ni kwamba kazi yangu ndio tegemezi langu kwa hapo baadaye kwasababu most of other business zinategemea kazi hii ya (BIT) ikiwemo wafanyabiashara na makampuni mbalimbali anasema na kuongeza.

“Watu wa taasisi za serikali na zisizo za serikali wanategemea sana watu kama mimi ili kuhakikisha taarifa za taasisi zinakua well managed na zinaenda vile ipasavyo halikadhalika na benki vile vile wanatutegemea” anasema.

Alaaa kumbeee!! Embu tuweke wazi hapa mtu akitaka kufanya kazi hii anatakiwa kusomea masomo gani?

“Kwanza anatakiwa awe na msingi kuhusiana na masuala ya computer awe anauwezo wa kuitumia angalau kidogo, awe anafahamu pia masomo ya biashara ikiwemo book-keeping na commerce pia” anasema.

Je Course ya BIT inahusika na nini?

“Course hii inahusisha mambo makuu mawili ikiwemo biashara pamoja na IT kwani inatoa wataalamu wa biashara na wa IT halikadhalika lakini hapa watu wanatakiwa kuwa na uelewa wa biashara ndiyomana course hii ikaitwa BIT” anasema

Kumbee eeeeh!! Sawaaa, Atham anaeleza sababu za yeye kuamua kusomea kozi hiyo

“Kiukweli ushawishi ni mimi mwenyewe utundu wangu ndiyo umenifikisha na kuweza kusomea kazi hii tangu mdogo kaka yangu kwa mara ya kwanza aliponunua computer nilianza kujifunzia hapo ndipo nikagundua kama computer inabeba mambo mengi sana na kuamua kusomea masuala haya” anasema.

Vipi kwa upande wako unafikiri jamiii inauelewa wa kutosha  kuhusiana na masuala ya  Technolojia ya habari ya biashara?

“Naweza kusema kuwa kwa kiasi asilimia 50 jamii inaulewa kwani sasa hivi technolojia imekua ikitumiwa na zaidi ya asilimia 60 katika jamii za watu wa Tanzania hata wazee pia niwatumiaji wazuri”

“Hata hivyo serikali pia mifumo mingi imekua inafanyika kwa njia ya Technolojia tofauti na hapo awali ile mifumo asili ya kuhifadhi taarifa kwenye madaftari sasa hivi ni tofauti technolojia inatumika sana kwenye sector mbalimbali”anasema.

Atham afunguka changamoto za kazi hiyo

“Upataji wa hizo kazi zenyewe unazozifanya kwasababu imekua ni kazi ambayo kila mtu anaifanya watu wengi wanafanyakazi hii tofauti zetu ni ule ubunifu na jitihada ndizo zitakazotusaidia kuepukana na changamoto hizo”

“lakini pia kuenda sambamba na technolojia kwani technolojia inakwenda mbio sana na kila siku technolojia mpya zinabuniwa sasa watu kubadilika kutoka technolojia za zamani kutumia mpya ukiimbia kampuni au taasisi Fulani wataona kama vile unataka kuwaibia  hapo ndiyo changamoto”anasema

Je unamshauri nini kijana anaetaka kufanya Kazi hii?!

“Ushauri pekee nitakaompa kijana anayetaka kufanya hii kazi ni kusoma sana, kufanya jitihada ya ziada ukiachana na ile anayoipata chuo au shule ukiachana na masomo ya chuo untakiwa kuwa mfatiliaji wa vitu mbalimbali ili uweze kuifanya hii kazi”anasema

Wewe ni Mtu wa aina gani!,  unapenda nini na kipi hupendi maishani mwako?

“Mimi ni mtu ambaye napenda sana kusoma, mimi ni mtulivu, napenda kukutana na watu mbalimbali  ili kujifunza, napenda kusafiri, napenda pia kusaidia watu kwenye jamii lakini pia napenda sana kufanya kazi”anasema na kuongeza

“.Vitu ambayo visivipendi sipendi choyo yaani vile unafanya kitu halafu mtu anachukia lile zuri unalolifanya, sipendi kumuona kijana mwenzangu anaharibikiwa kimaisha”anasema.

Nani unamshirikisha katika kufanya maamuzi kwenye jambo lako

Unapofika wakati wa kufanya maamuzi kwenye jambo lako lolote

“Katika kufanya maamuzi huwa kwanza nachanganua mimi mwenyewe lakini pia nachukua mawazo ya watu kwani naamin kupitia mawazo ya wengine unaweza kupata muelekeo mzuri wa jambo lako”

Akaaah!!! Vizuri malengo yako yapi hasa?

“kwasasa nataka nitumie ujuzi wangu wa biashara na technolojia ya habari katika kukuza biashara ambazo mimi mwenyewe nimeanzisha na nasimamia biashara ya Restaurant mgahawa ambao niumeuanzisha from the scruch nataka niusimamie kupitia taaluma yangu ambayo nimeisomea nataka nifanye kitu chakwangu na kiwe kikubwa.”anasema

Ebwana eeeh!! Unaambiwa hayo ndiyo malengo makuu ya kijana Atham ambaye bado nimwanafunzi kama wewe niambie unafikiri nawewe kufikia malengo yako kuna ugumu? Hapana ni komaa na unachokipigania ni jumatatu ya makala ya kazi tupige kazi mzee baba!!!!!!!!!!.






Comments 1


  • Awesome Image
    Afrah

    Kila la kheri kwako Atham kijana mpambanaji natumai kupitia taaluma yako vijana weng wa rika lako watafaidika na watakua na wigo wa kukufuata ,Bless sana Ma boy☺

Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post