Amazing things your phone can do

Amazing things your phone can do

Surprise!!! Mambo vipi? Kila mtu ana matumizi yake binafsi kwenye simu yake au siyo bhana? je una fahamu uwezo wa simu yako ulivyo mkubwa, maybe kuliko hata ulivyodhania?

Leo kwenye smartphone nakupa vitu ambavyo simu yako inaweza kufanya. Mbali na kupiga simu, kuperuzi mitandaoni kama vile Facebook, Instagram hata kutuma ujumbe WhatsApp, fahamu tu kuwa simu yako ina mambo mengi sana inayoweza kufanya.

Moja ya matumizi extra ambayo simu yako inaweza kufanya ni hizi hapa bwana:

Zuia watu kutumia programu katika simu yako

Unajua bhana kila mtu kwenye simu yake ana sehemu zake ambazo hatamani kuingiliwa privacy yake, sio kila unaemuazima simu yako ana nia njema na wewe, angalia hili kwanza.

Unaweza kutumia program kama vile Applock ambayo inazuia mtu kuingia katika program ya Google PlayStore, ili asiweze kupakua program yoyote ile bila wewe kujua.

Vilevile kama una simu aina ya Iphone unaweza kutumia program ya Notes, katika kitufe cha alama ya jumlisha, tumia Scan documents, hivyo unaweza kutumia Google drive kisha bonyeza kitufe cha save mambo yatakua tayari.

 

 

Unaweza kusoma text zako na emoji

Hapa sijui tumefahamiana kwanzaa au vipi? Raha ya kuchat lazima uonyeshe vitendo bhana. Ukifurahishwa unatakiwa kuonyesha hali ya furaha, hata ukichukizwa pia uwezo upo kwenye simu yote haya unaweza kuyafanya.

Lakufurahisha zaidi iwapo unatumia Iphone una uwezo wa kuchonga na ‘Siri’ ukamwambia siri kuna lolote limeingia leo kwenye simu yangu? Na akakupa majibu.

Kwa wale wanaotumia android usiwaze sana, unaweza kutumia program kama vile ReadItTome ukafurahia maisha.

 Unaweza kupiga picha wakati huo huo ukarecord video

Aisee hivi unajua kuwa unaweza kupiga picha huku ukiwa anajichukua video? Linawezekana hili kwa kutumia simu yako mwenyewe bila hata kutaka msaada pembeni kwa kutumia Android au iPhone.

 Piga picha huku ukirecord gusa skrini yako unaporecord video iwapo unatumia iphone unatakiwa kubonyeza mahali unapotumia kupiga picha yaani kile kitufe cheupe karibu na kitufe cha kurekodia video.

Lakini picha hizo haziwezi kuwa kali sanaa ukilinganisha na ile ungekuwa unapiga picha ya kawaida, ila itakusaidia tu ukiwa unapiga picha kwa wakati huo unaweza ukahifadhi tukio hilo.

Kuwa mjanja bhana nimekupa hiyo endelea kuenjoy kupitia smartphone yako. Have a good day!

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post