Mahakama nchini Libya siku ya jana Jumatatu ilitoa hukumu ya kifo kwa wanajihadi 35 waliokutwa na hatia ya kupigana pamoja na kundi la Islamic State katika nchi hiyo iliyopo Afrika kaskazini.
Watuhumiwa waliungana na IS wakati wa machafuko baada ya kuangushwa kwa utawala wa dikteta Moamer Kadhafi, moja ya chombo cha habari kilichokuwa katika mahakama hiyo kilisema.
Washtakiwa hao walikuwa Wapalestina, Wasudan na Walibya. Wote walikuwa wamewekwa kizuizini tangu mwezi Desemba mwaka 2016 na kukutwa na hatia ya kujiunga na kundi la kigaidi, pamoja na mauaji.
Huku washtakiwa wengine 13 walihukumiwa vifungo vya maisha, baada ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa mwezi Agosti mwaka jana katika mji wa magharibi wa Misrata.
Leave a Reply