Zifahamu kazi zinazolipa zaidi

Zifahamu kazi zinazolipa zaidi

Watu wengi wamekuwa wakisoma kwa malengo maalum. Japo wengi huchagua kusomea taaluma fulani kwa kuwa ina soko kubwa la ajira na kuwa na malipo mazuri ya mishahara.

Hakuna anayependa kusomea taaluma ambayo anajua wazi kuwa haitomnufaisha katika maisha yake. hivyo vijana wengi wamekuwa makini sana katika uchaguzi wa taaluma ya kusomea.

Leo katika karia tuna utafiti ambao umeonesha kazi mbili zinazolipa zaidi Tanzania.

Ripoti ya utafiti wa ajira na kipato ya mwaka 2016 (EES 2015) iliyochapishwa mtandaoni na Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) imeonesha kuwa sekta ya huduma za kibenki na bima ndiyo inayolipa zaidi nchini.

Utafiti huo umeonesha wastani wa kiwango cha chini zaidi cha mshahara wa wafanyakazi katika sekta ya fedha na bima kimepanda kutoka Milioni 1.198 kwa mwaka 2015 hadi Milioni 1.388 kwa mwaka 2016.

Imeelezwa kuwa sekta hiyo hutoa mishahara mizuri zaidi kulinganisha na sekta nyingine kutokana na uhaba wa wataalam, hali inayosababisha waajiri kuongeza kiwango cha mishahara kuwavutia wafanyakazi wenye sifa stahiki.

Kwa mujibu wa utafiti huo, wafanyakazi wanaojihusisha na sekta za utawala, ulinzi wa jamii ndio wako katika nafasi ya pili ya malipo ya juu Tanzania ambapo wana wastani wa mishahara kati ya Sh1.293 milioni kwa mwaka 2016 ukiwa umepanda kutoka wastani wa Sh997, 058 kwa mwaka 2015.

Hata hivyo imeelezwa kuwa bado kuna tofauti kubwa ya mishahara kati ya wanaume na wanawake kwa ujumla ambapo wanaume wanaonekana kuwazidi wanawake.

Huo ni utafiti wa mwaka 2016 lakini leo ni mwaka 2021, basi endelea kuwa nasi ili kuweza kujua ni kipi kimeibuka katika tafiti zitakazotolewa hivi karibuni kuhusiana na sekta hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post