Wakati baadhi ya wanawake wakitumia mbinu mbalimbali ili kupendezesha midomo yao, huku wapo wale wa kupaka vitu kama vile lips ticks na kufanya upasuaji wa midomo.
Wafahamu watu wa kabila la Mursi, ambao wanawake wa kabila hilo hutobolewa midomo yao ya chini wanapokaribia kuwa watu wazima na kisha kuvalishwa visahani vya udongo katika masikio na midomo yao kama urembo.
Licha ya kuufanya muonekano huo kama utamaduni wao, inaelezwa kuwa, mwanzo wanawake wa kabila hilo walilazimika kutobolewa midomo yao, ili kutowavutia wanaume wa kivamizi ambao walikuwa wakivamia jamii hiyo na kuchukuwa wanawake kwa kuwafanya mateka.
Ukubwa wa sahani katika mdomo ndiyo kigezo cha wanawake wa kabila hilo kuolewa haraka.Ili kupata mke wanaume wa kabila hilo halazimika kufanya pambano la kuchapwa fimbo, ili kuthibitisha nguvu zao kwa wanawake wanaotaka kuwaoa.
Kabila hilo la Mursi linapatikana katika eneo la bonde la Omo nchini Ethiopia na inaelezwa kuwa ni miongoni mwa makabila tajiri zaidi katika bonde hilo kutokana na idadi ya mifugo ambayo humilikiwa na kila mtu.
Leave a Reply