Njia za kuepuka uvivu kazini

Njia za kuepuka uvivu kazini

Waswahili wanasema ‘asiefanya kazi na asile’ basi na mimi naendelea kuishi katika msemo huo, kama kawaida yangu lazima tukumbushane kuhusiana na masuala mazima ya kazi katika nyanja mbalimbali.

 

Leo tutazungumzika tabia ya uvivu kazini hii imezoeleka sana katika kampuni kadhaa kwa baadhi ya wafanyakazi kutegea, mara tuu wanapoanza kuzoea kazi au ofisi fulani. Hapa nakujuza njia za kuepukana na uvivu mahala pa kazi.

 

  • ONGEZA UBUNIFU

Kwa kufanya hivi kutakufanya usiwe mvivu kazini ukiwa mbunifu na ukatumia njia mpya kukamilisha majukumu yako ya kila siku hii itakusaidia kila siku kuwa na kitu kipya katika akili yako, hivyo hautaona uvivu kwa kuwa akili yako itakuwa inawaza kubuni kitu gani cha kufanya.

 

Ili kufanikiwa lazima pia uweke au utengeneze mazingira ya kufanikiwa, ambapo ili uwe na uhakika wa kufanikiwa katika jambo unalolifanya inategemea misingi ambayo umejiwekea, kama kutambua umuhimu na msaada wa imani katika kufanikiwa kwako.

 

  • EPUKA KUGHAIRISHA KAZI

Asilimia kubwa ya watu wanapenda kughairisha mambo, kufanya hivyo kutakusababishia kuona uvivu wakati wa kufanya kazi yako na hii itapelekea kutokufanya kwa ufasaha na umakini.

 

  • TENGENEZA USHIRIKIANO KAZINI

Kuwa na mtandao wenye ushirikiano mzuri wa ku-share mawazo na marafiki wachapakazi itasaidia kupata mawazo mapya na itakupa hamasa ya kufanya kazi kuna msemo wanasema ‘ukikaa na waridi lazima unukie’ kuwa na urafiki na wafanyakazi walio mahodari wa kazi watakufanya ufikie malengo yako.

 

  • ACHA KUISHI BILA MALENGO

Mafanikio siyo kitu ambacho kinatokea kwa bahati mbaya lazima ujifunze kuwa na mipango madhubuti ya kufanikiwa, kuelekea kijiji cha mafanikio, kunahitaji kuwa na mikakati ambayo ukiitizama itakuonesha muda sahihi wa wewe kufanikiwa.

 

Malengo yanaweza kukufanya ufanye kazi kwa wakati na hautakuwa na muda wa kupoteza sikuzote ukijiwekea mpangilio katika maisha yako lazima utafanya kwa bidii zako zote ili ufanikishe jambo fulani, hasa ukiwa na watu wanaokutegemea.

 

  • PENDA UNACHOFANYA

Penda mipango yako penda kazi unayofanya ili kukuongezea msukumo wa ndani wa ufanyaji kazi itakusaidia kufanya kwa bidii bila kuchoka na muda wote utatamani uwe katika majukumu ya kazi.

 

  • WEKA RATIBA NA MIPANGO YA MAENDELEO

Hakikisha una ratiba ya kukuelekeza muda na ukomo wa kufanya mambo yako lakini pia mipango madhubuti na mikakati makini itakayokufanya ufikie mafanikio utakayo. 

Heshimu ratiba na mipango uliyojiwekea kwa kuhakikisha unafanya kila ulichopanga kwa wakati na uamini kwenye  maamuzi yako na unachokifanya ni sahihi, usifuate maneno au mawazo ya mtu mwingine, hii itakusaidia kufanya kazi kwa bidii, akili na kwa nguvu zako zote






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post