Njia ya kununua bidhaa zenye ubora kupitia aliexpress

Njia ya kununua bidhaa zenye ubora kupitia aliexpress

Na Tanzania Tech

Utaweza kupata bidhaa bora na zenye kufanana na picha ya bidhaa usika

Kwa sasa ni wazi kuwa watu wengi zaidi wamekuwa wakifanya manunuzi mtandaoni, lakini ni wazi kuwa kuna wakati bidhaa unayopata ni tofauti na ambavyo ulitegemea kwani unakuta bidhaa haina ubora na ni tofauti kabisa na ambayo inaonekana kwenye picha.

Kuliona hili leo nimekuletea njia mpya ambayo itakusaidia kuweza kupata bidhaa bora kwa urahisi kupitia mtandao wa Aliexpress. Njia hii ni bora na inaweza kuwa msaada mkubwa sana kwako kama umekuwa mtumiaji au ukifanya manunuzi kwenye mtandao wa Aliexpress.

Basi bila kupoteza muda moja kwa moja twende kwenye njia hii, kwa kuanza moja kwa moja download app kupitia link hapo chini baada ya hapo hakikisha pia unayo app ya Aliexpress kwenye simu yako. Kama unazo app zote mbili basi endelea.

Baada ya hapo fungua app ya Aliexpress, kisha moja kwa moja tafuta bidhaa unayotaka kununua, baaada ya hapo bofya kitufe cha share kilichopo juu upande wa kulia kwenye app ya Aliexpress.

Baada ya hapo utaweza kuona menu mpya imefunguka kwa chini, moja kwa moja kwenye Menu hyo bofya kitufe cha More ambacho ni cha mwisho kutoka kulia.

Baada ya kubofya kitufe cha More, moja kwa moja itafunguka sehemu yenye App mbalimbali, changua app uliyo download hapo awali.

Baada ya hapo subiri app hiyo itafunguka na moja kwa moja utaweza kuona ukurasa kama huo hapo chini, ukurasa huo utakuwa na bidhaa yako uliyo chagua kupitia Aliexpress.

Kwenye ukurasa huu bofya sehemu iliyo chorwa kamera iliyopo mwanzo upande wa kushoto na kuitia ukurasa huo utaweza kuona maoni ya na picha za watu walio nunua bidhaa hiyo. Hiyo itakusaidia kama kuna malalamiko yoyote utaweza kuona kwa haraka pia utaweza kuona picha za bidhaa hizo ambazo zimepigwa na watu ambao tayari wamenunua bidhaa hizo.

Sehemu ya pili itakusaidia kuona kama muuzaji wa bidhaa hiyo ana aminika, unaweza kuona kwa kuangalia rangi ya asilimia, kama asilimia ni ndogo na zina rangi nyekundu basi muuzaji wa bidhaa hiyo sio muaminifu na amekuwa akiuza bidhaa zisizo na ubora.

Sehemu ya pili itakuonyesha kupanda na kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo, unaweza kuona bei hiyo ili kuangalia kama bidhaa hiyo imekuwa ikipanda au ikishuka.

Sehemu inayo fuata itakusaidia kuweza kuona bidhaa ambazo zinafanana na bidhaa hiyo, yaani kama ni saa basi utaweza kuona saa zenye sifa kama hizo.

Kwa kufanya hivyo utaweza kuona kama bidhaa hiyo inafaa kwa manunuzi au kama haifai, kama umeona bidhaa hiyo inafaa unaweza kuendelea kwa kununua bidhaa hiyo kupitia mtandao wa Aliexpress au unaweza kubofya sehemu ya Open in AliExpress kununua.

Pia unaweza kuwasha Notification kwenye sehemu ambayo itakusaidia kuweza kujua bei ya bidhaa hiyo inaposhuka au inapo panda.

Kwa kufanya hatua hizo zote utaweza kupata bidhaa bora na ambazo zinafaa kwa matumizi, unaweza kutumia njia hii muda wowote ambao unataka kununua bidhaa kupitia mtandao huo. Kizuri ni kuwa app hii haina matangazo na ni bure kabisa kutumia.

Aiseee kwa leo niishie hapa ihope utakua umenipata vyema kabisa tukutane next week kwenye ukurasa wetu huu huu wa makala za Technolojia have a nice day watu wangu wa nguvu!!!.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post