Mwandishi wa habari jela miaka 5

Mwandishi wa habari jela miaka 5

Mahakama ya rufaa nchini Iran imemhukumu kifungo cha miaka mitano mwanaharakati maarufu na mwandishi wa habari Golrokh Iraee ambaye amekuwa akizuiliwa tangu kukamatwa kwake mwanzoni mwa vuguvugu la maandamano nchini humo.

Iraee alikataa kushiriki katika usikilizwaji wa kesi yake kwenye mahakama ya rufaa akishutumiwa kushiriki katika mikusanyiko haramu na kukiuka usalama wa taifa, akisema hakutambua uhalali wa mahakama hiyo.

Mwanaharakati huyo alikamatwa Septemba mwaka jana katika msako wa polisi akiwa nyumbani kwake mwanzoni mwa maandamano yaliyochochewa na kifo cha Mahsa Amini, ambaye alikuwa amezuiliwa kwa madai ya kukiuka sheria kali za mavazi kwa wanawake.

Iraee, ambaye alikuwa katika gereza la Evin kwa siku 280 alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela na mahakama ya Tehran.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post