Marekani, Mexico zaonya kuhusu mlipuko wa fangasi

Marekani, Mexico zaonya kuhusu mlipuko wa fangasi

Nchi ya Marekani na Mexico zimelitaka shirika la Afya Duniani (WHO) kutangaza dharura ya afya ya umma kutokana na mlipuko wa fangasi ya uti wa mgongo unaohusishwa na shughuli za upasuaji wa urembo(plastic surgery) katika nchi hizo.

Lakini vituo vya kudhibiti na kuzuia magonjwa (CDC) vilisema watu wawili ambao walipata upasuaji unaohusisha kuchoma ganzi ya kuzuia maumivu wamekufa kwa ugonjwa wa uti wa mgongo.

CDC ilisema tayari imewatambua watu 25 nchini Marekani wenye visa vinavyoshukiwa au vinawezekana vya homa ya uti wa mgongo.

Aidha raia wengi nchini Marekani husafiri hadi Mexico kwa ajili ya taratibu za urembo kama vile kunyonya mafuta (liposuction) kuongeza matiti na kunyanyua makalio ya Kibrazili, ambayo yote yanahitaji kudungwa sindano ya ganzi kwenye eneo karibu na safu ya uti wa mgongo.

Dallas Smith wa CDC alisema kuwa dawa zinazotumiwa wakati wa ganzi katika mlipuko wa sasa zinaweza kuwa zimeambukizwa ama kwenye epidural yenyewe au katika dawa nyingine ambazo huongezwa kwa kushirikiana wakati wa upasuaji kama vile morphine.

Oktoba mwaka jana, kundi la dawa ya ganzi ya kawaida inayotumika kwa upasuaji kama vile uzazi wa upasuaji iligunduliwa kuwa imeambukizwa na fangasi sawa, na kusababisha vifo vya watu 39 katika jimbo la Mexico la Durango.

Chanzo  BBC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post