Maadhimisho ya siku ya nukta nundu (Braille) Duniani

Maadhimisho ya siku ya nukta nundu (Braille) Duniani

Kila Januari 4 ya kila Mwaka, Dunia huadhimisha Siku ya Nukta Nundu kwa lengo la kuongeza Ufahamu kuhusu  haki za binadamu kwa wenye Ulemavu wa Kuona, na Uoni Hafifu.

Madhumuni ya Siku hii ni kuhamasisha Umma kuhusu thamani ya ‘Nukta Nundu”  kama njia ya Mawasiliano kwa Wenye Ulemavu wa Kuona

Aidha Nukta Nundu (Braille) ni Kiwakilishi cha kugusa chenye Alama za Namba na Alfabeti, ambapo Herufi na Namba zinawakilishwa na Nukta 6. Pia kuna alama za Hisabati, Muziki, na Sayansi. Na hii hutumika Zaidi katika maofisi, vyuo na shule kwa ajili yakuwawezesha kufanya majukumu yao kama watu wengine.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post