Kilichofanya Lupita Nyongo asiongee lafudhi ya Kikenya

Kilichofanya Lupita Nyongo asiongee lafudhi ya Kikenya

Nyota wa Hollywood Lupita Nyong’o, amefunguka namna alivyoamua kuacha kuiga lafudhi ya Kimarekani na kurudi kwenye lafudhi yake ya asili ya Kikenya licha ya kuwa aliificha kwa kipindi kirefu.

Lupita wakati akizungumza katika kipindi cha kwanza cha podcast yake mpya ‘Mind Your Own’ alisema ili kupata nafasi zaidi na waigizaji wengi wa Hollywood, aliamua kuzungumza kama Mmarekani na kuficha lafudhi yake ya Kikenya. Hata hivyo hali hiyo ilidumu hadi usiku wa ziara ya waandishi wa habari kwenye filamu ya '12 Years a Slave' (2013).

“Walikuwa hawajawahi kunisikia nikizungumza kwa lafudhi yangu ya Kikenya,” alisema

Alisema kwa ushawishi wa mama yake na ulimwengu kumpokea katika hali yake ya kweli, aliwasiliana na wawakilishi wake na kuwaambia kwamba anataka kurudi kwenye lafudhi yake ya asili na kutuma ujumbe kwamba kuwa Muafrika inatosha.

Ikumbukwe Lupita alizaliwa tarehe 1 Machi 1983, na alijulikana zaidi baada ya kuigiza katika filamu ya "12 Years a Slave," ambayo ilimletea tuzo ya Academy Award kama Mwigizaji Bora wa Pili lakini pia mwanaharakati wa haki za binadamu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post