Kazi ya hoteli katika kuhudumia wateja na changamoto zake

Kazi ya hoteli katika kuhudumia wateja na changamoto zake

Kazi ya hoteli inahitaji uvumilivu, subira, uaminifu, kujituma na unyenyekevu. Ni kazi inayohitaji kujitoa sana na kuwa na utu na nidhamu ya hali ya juu. 

Hebu fikiria soda mtaani inauzwa shilingi 500 lakini kwenye hoteli za hadhi ya nyota 4 na 5 inauzwa kati ya shilingi 3000, 4000 na 5000. 

Beer zinauzwa kati ya shilingi 4000, 5000, 7000 mpaka 10000 katika hizo hoteli za nyota 4 na 5, sasa jiulize kinachomleta mteja hapo kutumia hela kubwa kiasi hicho ni kitu gani?

Wateja wanatarajia kupata huduma ya kiwango cha juu, mandhari nzuri, usafi wa kiwango cha juu, usalama na wahudumu wenye weledi na wanaojua kujali wateja.

Kwenye huduma za Hotel wahudumu kwa maana ya waiters na waitresses wanayo kanuni moja inaitwa 3P.

Kwa maana ya… 

 

  1. Pen 
  2. Paper
  3. Patience 

 

Lazima uwe na kalamu na karatasi au wenyewe tunaita captain order kwa ajili ya kuandika kile anachotaka mteja na kuwa na subira au uvumilivu na unyenyekevu.

Baadhi ya wateja wanakuwa na kiburi na majivuno kwa sababu ya pesa zao au kiburi tu cha kujiona wao ni bora na kutaka pengine sifa na kutambuliwa.

Kwa hiyo mhudumu anapaswa kumsaidia bila kumuonyesha dharau au kumfedhehesha hususan kama yuko na wenzake.

Kwa mfano wanaume wanaowatoa wanawake zao kwa kuwaleta kwenye hotel kubwa wana kawaida ya kujimwambafai wakati hawajui hata kusoma menu, sasa mbele ya mwanamke anaweza kujikwenza na kuonyesha ni mwenyeji kwenye maeneo hayo na kuagiza chakula ambacho hakiendani na mazingira husika.

Hii unafanya kwa uangalifu mkubwa na unapaswa kujenga urafiki ili akuamini.

 

Changamoto nyingine ni matumizi ya cutleries.

Kwa upande wa cutleries (curtleries ni nyenzo zinazotumika katika kula chakula hususan hotelini ambazo ni uma, visu na vijiko, kwa ujumla wake huitwa hivyo kwa lugha ya wenzetu)

Zipo za aina nyingi zinapangwa mezani na kile mteja atakachoagiza kinaweza kusababisha zikaondolewa na kuwekwa nyingine. Kuna visu vya nyama, samaki na chakula bahari (seafood) kwa mfano crab au lobster.

Utaalamu wa namna ya kuvitumia.

Kula kwa mkono inaruhusiwa lakini kuna namna ya kushika na kuna vitu haviruhusiwi kuliwa kwa mkono, watu watakushangaa. Jukumu la waiter au waitress ni kumuelewesha mteja kwa namna ambayo itamfanya asijisikie vibaya.

Kwa bahati mbaya hatuna vyuo vya mtaani vya kufundisha kitu kinaitwa ‘Etiquette’ yaani ‘ustaarabu’. Lakini mtandao wa YouTube umerahisisha ukitaka unaweza kujifunza kupitia huko.

Lakini kingine kama kuna buffet namna ya upakuaji ni mtihani kwa watu wengi hawajui. 

Naomba nitoe darasa kidogo....

Kuna wakati wahudumu wanapata wakati mgumu kuwahudumia wateja lakini kama wakijenga mahusiano mazuri na wateja basi hawatapata taabu kuwahudumia.

Kwa upande wa buffet lunch bila kinywaji bei ni kati ya TZS 30,000 mpaka TZS 50,000 na dinner ni kati ya TZS 40,000, 50,000, 60,000 mpaka 90,000 kwa mtu mmoja katika hizi hoteli za nyota 4 na nyota 5.

Wakati wa kula mteja anatakiwa aanze kutumia uma na kisu kutokea nje kwenda ndani kama vilivyopangwa mezani.

Uma na kisu vya kwanza ni kwa ajili ya salad au starter na kijiko ni kwa ajili ya supu kama mteja ataamua kunywa supu.

Uma na kisu vya mwisho ni kwa ajili ya main course yaani mlo mkuu.

Mara nyingi watu mchana hawapendi kula desert lakini wakitaka wanapangiwa uma na kisu tena.

Meza ya dinner uma na visu vinavyowekwa juu ni vya desert kwa sababu usiku wengi hula desert.

Kama ilivyo menu ya chakula, kuna starter ambapo zinakuwepo orodha ya aina za supu na salad. 

Kisha snacks na pasta na mwisho main course.

Nikisema snacks yaani light food au vyakula nyepesi vya haraka namaanisha baguette, burger, chicken wings, chicken finger, fish finger, vegetable spring rolls nk.

Sasa kwenye buffet ukitaka kupakua chakula unatakiwa kufuata mpangilio huo

Starter - soup au salad au vyote unachukua kimoja baada ya kingine. Uzuri ni kwamba buffet unarudia kupakua chakula mara nyingi utakavyo na vyakula haviishi vinakuwepo muda wote.

Baada ya kula salad na supu au kimojawapo ndipo hufuata main course ambapo kuna vitu vingi kama, wali, samaki, nyama, na mazagazaga mengi tu, lakini inatakiwa ujue kuremba sahani kwa kuweka kidogo kidogo kwa mpangilio na usijaze sahani kwa sababu unalipa 80,000, utarudia mara nyingi utakavyo. Pakua kidogo kidogo kwa ustaarabu. 

Ukipakua kwa kiasi na kurudia rudia unaweza kula chakula kingi kwa nafasi kwa sababu unakula kwa utulivu.

Naomba niwamegee siri. 

Kabla ya kupakua chakula fanya survey kidogo, inaruhusiwa kukagua vyakula vyote kwenye buffet na unaweza  kuuliza maswali kwa ufafanuzi wapishi wapo kwa ajili ya kukusaidia.

Ukifanya Survey utajua ule nini na uache nini, lakini usipojua utajikuta unajaza sahani kwa sababu kila unachoona unakitamani. Hapa sizingumzii buffet za harusini au sherehe mnapopangiwa chakula na mpakuaji.

Uliza maswali tulia usiwe na papara. Kama umejua chakula unachotaka pakua siyo lazima ule vyakula vyote utavimbiwa.

Kosa wanalofanya Watanzania wenzangu ni kuchanganya starter, main course na dessert kwenye sahani moja yaani chakula kina chumvi na dessert ina sukari sasa hapo unapata ladha gani?

Mtu kapakua wali, kuku, samaki, nyama halafu salad kisha bonge la kipande cha keki au matunda juu. Ukila utatapika na hata ukiangalia sahani utaona kama inakufokea. 

Sikatai unaweza kuchukua main course na salad kidogo lakini usijaze michuzi kwani vinegar na mayonnaise na mchuzi wa curry wenye pilipili utatengeneza atomic bomb!

Naomba kwa leo niishie hapa, Nitaendelea kutoa darasa zaidi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Shaban Kaluse

A Sales and Marketing in the hospitality Industry and also a freelance journalist, writing about love and relationships and educative articles which aims for youths, every Tuesday on Mwananchi Scoop.


Latest Post