Kampuni inavyowalazimisha wafanyakazi kwenda nyumbani kwa muda

Kampuni inavyowalazimisha wafanyakazi kwenda nyumbani kwa muda

Kampuni ya teknolojia ya mawasiliano imeweka programu ya software inayowakumbusha waajiriwa kuondoka kazini kwa muda uliopangwa.

Tanvi Khandelwal, mwenye umri wa miaka 21, alishangaa hivi karibuni aliporejeshwa wakati skrini yake ya kompyuta ya kazi ilipowaka vimulimuli vya rangi nyekundu vikiwa na maandishi.

“Muda wako wa kazi umeisha mfumo wa kompyuta utazima katika kipindi cha dakika 10, Tafadhali nenda nyumbani” computer iliandika

Khandelwal ambaye alikuwa amejiunga na kampuni hiyo, katika kitengo cha maslahi ya wafanyakazi siku chache zilizopita, baadaye alibaini kuwa ujumbe huo ulikuwa umewekwa na muajiri wake mpya ili kumfanya azime kompyuta yake kwa muda na kumaliza kazi kwa muda uliopangwa.

Ni mmoja wa wafanyakazi 40 wa SoftGrid Computers kampuni mpya ya teknolojia ya India makao yake katika jiji la Madhya jimbo la Pradesh ambao hupata jumbe za kila siku za kuzima kompyuta zao kila siku, dakika 10 kabla ya muda wao wa kumaliza kazi kufik Saa moja kamili jioni kompyuta zao hujizima zenyewe.

Shweta Shukla, Mkurugenzi mkuu na muasisi wa SoftGrid, anasema kwamba ujumbe huo ni sehemu ya juhudi za kampuni za kuwasaidia wafanyakazi kufurahia kazi na maisha yao nje ya kazi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post