I hope mko good watu wangu wa nguvu, kama mnavyojua wanavyuo wengi wamemaliza mitihani na wako mbioni kupeleka CV zao katika makampuni mbalimbali sasa leo nakusogezea kitu ambacho kitakusaidia ili upate kazi kwa haraka, najua mnadanganyana na kutishana mambo mengi sana kuhusiana na usaili so ungana na mimi ili usipate hofu tena.
Karibu kila mtu hupata wasiwasi wa kiwango flani kabla na wakati wa usaili, ni kawaida kuhisi wasiwasi kabla na wakati wa usaili au katika jambo lolote ambalo ni mara yako ya kwanza kulifanya kwa sababu unajiona una karibia kuchunguzwa muonekano wako, tabia yako, unachosema na namna unavyosema kabla ya mwajiri kuamua kukupa au kukunyima ajira.
Na siku zote wasiwasi kupitiliza unaweza kuharibu utulivu na ufanisi wako kiasi cha wasaili kusumbuliwa na tabia zinazoweza kuletwa na wasiwasi huo na kushindwa kutilia maanani uwezo na sifa zako.
NJIA AMBAZO ZITAKUFANYA KUONDOA HOFU NA WASIWASI KATIKA USAILI
1. ANZA KWA KUJIANDAE
Maandalizi ni njia bora ya kushinda wasiwasi maandalizi yakutosha yatakujengea kujiamini na hivyo kutengeneza nishati chanya kwenye akili yako.
Maandalizi ya usaili yanatakiwa kuandaliwa mapema mfano kujiandaa kiakili na kupunguza presha ya maswali utakayokwenda kuulizwa, cha muhimu ni kuandaa CV viziri na kujua ulicho kiandika katiak wasifu wako.
2. JIKUBALI
Watu wengi wanadhana ya kuwa usaili wa kazi ni kama mahojiano na polisi. Wanahisi hawatakiwi kabisa kufanya kosa kwa hofu ya kuhukumiwa.
Ni muhimu kukumbuka kuwa wewe pia unamuhoji mwajiri ili kuona kama majukumu na mazingira ya kazi ni sawa kwako.
Kuufikiria usaili kama mtihani kunaweza kuchochea hisia za wasiwasi na hofu, fikiria usaili kama mazungumzo kati ya watu wawili ambao wanajifunza kuhusu kila mmoja. Hivyo basi kitu cha kuzingatia zaidi ni kujiamini usiangalie mko wa ngapi katika usaili wala kuskiliza maneno ya watu kuhusu kushindwa.
3. KUFIKA MAPEMA SIKU YA USAILI
Jipe muda wa kutosha wa kuelekea kwenye usaili, toka nyumbani mapema iwezekanavyo ili foleni au hali ya hewa mbaya isikufanye kutofika kwa wakati, na ukishafika chukua dakika chache kujiandaa.
Kufika kwa wakati ni jambo zuri lakini usiingie mahali patakapo fanyia usahili dakika 20 kabla ya usaili, na kama unasubiri eneo la mapokezi zingatia weledi, utulivu wako maana kuna baadhi ya waajiri hupendelea kuwauliza watu wa mapokezi kuhusu matendo yako.
4. TABASAMU
Hofu husababisha kupumua kwa haraka na huweza kuathiri matamshi na sauti yako, kabla na wakati wa mahojiano kumbuka kwamba kuvuta pumzi rahisi sana kunaweza kufanya mengi kutuliza hisia, hofu na ku-panic.
Kuwa na wasiwasi kwenye usaili ni jambo moja lakini kumuonyesha msaili kwamba una wasiwasi ni jambo lingine Hivyo, kutabasamu kutasaidia angalau kuondokana na sura ya hofu kwenye uso wako, na hivyo wasaili wasiweze kugundua wasiwasi ulionao.
5. KUJIAMINI
Hata kama hujisikii ujasiri unaweza kukopa kwa kutumia lugha ya mwili Simama au kaa moja kwa moja, na mabega yako yakiwa nyuma. Hakikisha unatazamana usoni na wasaili wakati wote wa mahojiano, bila kusahau kutabasamu.
Pia, matumizi ya mikono na ishara wakati wa kuzungumza kunaweza kukuonyesha kama mtu unayejiamini. Kumbuka kuwa unapojiweka kama mtu mwenye ujasiri utaanza kujisikia jasiri zaidi kweli.
6. JIKITE KWENYE UWEZO WAKO
Usifanye kosa la kuvaa utu wa bandia, fikiria juu ya kila kitu kinachokufanya uwe mfanyakazi mzuri ikiwemo elimu yako, uzoefu wako na sifa binafsi, Kumbuka kwamba mpaka mwajiri anakuita kwenye usaili tayari ameona sifa zako nzuri, hivyo wasaili wananza na hisia nzuri kuhusu wewe.
Fikiria jinsi udhaifu wako unaweza kugeuka kuwa nguvu. Kwa mfano, ikiwa una tabia ya kukubali miradi mingi mara moja, basi unaweza kusema hilo litakuwa na manufaa kama utajifunza kuweka vipaombele na kupanga kazi zako.
7. ELEWA KUWA KUNAKUPATA NA KUKOSA
Sio jambo la kufurahisha kutopita kwenye usaili, lakini hutokea kwa kila mtu. Hivyo usijiadhibu kama usipofanya vizuri badala yake, fikiria juu ya kile unachoweza kujifunza kutokana na uzoefu ulioupata na ujitayarishe kwa fursa zitakazofuata.
Haijalishi nini kitatokea usaili utakupa uzoefu wa kujifunza ambao utakufanya uwe mgombea wa kazi bora na mkali wa usaili siku za usoni.
Leave a Reply