Jinsi ya kukabiliana na ushindani katika biashara ya saloon

Jinsi ya kukabiliana na ushindani katika biashara ya saloon

Watoto wengi wa mjini wanapenda sana kupendeza ndugu yangu, jaribu hii fursa ujionee maajabu sio kama nakutania ila waswahili wenyewe wanasema jaribu utakuja nishukuru badae hahahahah!

Kama unavyo jua jiji sasa limezungukwa na vyuo kila kona na kama unavyo jua wanachuo wanavyopenda kupodoka yaani kupendeza, kama huna ajira ungana nami ili ujikwamue kimaisha ili usiwe beki tatu.

Utunzaji wa nywele ni kitu cha kila siku kwa kila binadamu hapa sasa sinzungumzii wanawake peke yake hadi wakaka, Kwenye jamii yetu kila mtu anajali muonekano wake Nywele zinaongezea muonekano mzuri Na kukufanya uvutie zaidi

Kama unaweza kuhesabu gharama ulizotumia kwa mwaka mzima kutunza nywele utashangaa kwa kiwango kikubwa ulicho tumia bila mwenyewe kujua, Biashara ya salon zipo kila mahali lakini leo tutajifunza jinsi gani unaweza kukabiliana na ushindani huo na kumiliki idadi kubwa ya wateja. Kwanza ili biashara yoyote iweze kudumu kwanza inabidi uwe na msimamo na ujitoe sio biashara imetetereka kidogo basi umeacha jifunze kuwa mvumilivu 


KWANINI UFUNGUE BIASHARA YA SALOON

>Biashara ya salon unaweza kutenga muda wakufanya huku ukiwa na shughuli nyingine kama vile kuuza Nywele(wigs) mafuta ya Nywele kuuza nguo za maharusi na kukodisha pia Biashara hii unaweza kuiendesha ukiwa nyumbani.

>Hauhitaji kubuni bidhaa yako binafsi kwasababu kila siku mitindo mipya inatoka mitandaoni cha muhimu niwewe kufatilia mitandao ya kijamii ili kujua misuko inayo trend.

>Ni biashara ambayo wewe mwenyewe ukiweeka vizuri na kuwa mbunifu ndivyo wateja watakavyo miminika(kujenga urafiki na mteja)

 

JINSI YA KUFANIKIWA KATIKA BIASHARA YAKO

  • Unatakiwa uwe na ujuzi mzuri wa salon Kama wewe ni kinyozi ama msusi utakiwa uwe na utaalamu wa nywele hivyo utatakiwa uwaone watu wenye uzoefu katika maswala haya au kwenda kusomea maana siku hizi college ziko kila kona
  • Uwe na ukarimu kwa wateja yaani kuwa mchangamfu na wateja wako sio mteja kaja anakuuliza umenyamaza kimya mood zako mbaya ziweke pembeni na biashara yako
  • Unatakiwa kuwatawala washindani wako inabidi ujue mapungufu ya saloni zao na pia nini kinawaimarisha katika saloni zao na ndio utafaidika zaidi kwa huduma nzuri kwa wateja wako.
  • Chagua sehemu sahihi ambayo ni sehemu yenye mzunguko na wa watu, Watu wengi hukosea kuchagua sehemu sahihi ambapo wateja watakuwa na urahisi wa kufika kwa urahisi
  • Kuweka mazingira safi katika eneo la biashara yako, kama unahitaji wateja wajae katika saloon yako jua kuwa watu wengi wanapenda usafi wa kila kitu kuanzia vifaa na huduma zako kwa ujumla
  • Kuweka punguzo la bei ili saloon yako iweze kufanikiwa lazima kuweka bei rafiki ambayo haitakuumiza wewe wala mteja hii itakusaidia zaidi katika kumsoma vizuri mteja wako na kuto kumpoteza, mteja mwengine ukimtajia pesa kubwa basi ndo umempoteza huto muona tena siku nyingine.
  • kujiunga na mitandao ya kijamii kama vile Instagram na Facebook ili kutuma picha za kazi zako unazo zifanya na watu waweze kuzitambua na kufanikiwa kupata wateja wa sehemu mbalimbali

Haya sasa wafuatiliaji wa Mwananchiscoop natumai umejifunza kitu, anza sasa bado haujachelewa jitoe kwa ajili ya kile ukipendacho katika biashara yako usisahau kukoment na kushare ili na wengine waweze kujifunza na kufanya biashara zao kuwa bora zaidi.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post