Hofu ya kuzeeka Wasichana Kuolewa na yeyote

Hofu ya kuzeeka Wasichana Kuolewa na yeyote

Hivi sasa watafiti wengi wameonyesha kukubaliana na jambo hilo. Wanasema kwamba, wasichana wengi hubabaika na kufanya mambo yenye kuwaumiza kutokana na hofu kwamba, muda unakwenda haraka na watazeeka. Lakini pia huamini kwamba, starehe zitaisha.

Watafiti hao wanasema, kutokana na maumbile ya wanawake, ambapo miili yao hupevuka haraka, wengi huhofia sana umri. Wamebaini kwamba, mwanamke anachukia sana kuambiwa amezeeka au hujihami zaidi kuliko mwanaume asionekane kwamba, amezeeka. Kuzeeka kwa wanawake walio wengi kuna maana ya kuchusha na kutokupendwa tena.

Mwanamke anapofikia umri wa miaka 25 huanza kujiuliza kuhusu kuolewa, lakini pia huanza kujiuliza kuhusu watoto. Kama hajaolewa, hana mchumba au anahisi kutokupata mtu anayeamini atamfaa, huanza kuhofia. Anapofikia umri huo huanza kujiuliza pia kuhusu watoto.

Hofu za maisha ya upweke ya baadaye humjaa na kumfanya kuanza kubabaika. Ni katika kubabaika huko, ndipo ambapo huweza kufanya mambo ambayo watu wengine hujiuliza ni kitu gani kimemsibu. 

Kwa kuhofia kuchelewa kuolewa au kutoolewa kabisa, anaweza kumkubali mtu ambaye vinginevyo asingekubali kuwa naye kama mume. Kwa hofu ya kuingia kwenye umri mkubwa akiwa hana mume, humbeba yeyote.

Katika mazingira kama haya ndipo ambapo unakutana na wale ambao huolewa kwa madai ya kuondoa mkosi. Anachotaka ni kuolewa na mwanaume yeyote, ili mradi ionekane kwamba, maishani mwake naye alishawahi kuolewa.

Kuna wengine ambao huamua kuzaa na mwanaume ambaye anajua hataweza kumwoa. Hapa wengi huzaa na waume za watu. Inazidi kuelezwa kwamba, kubabaika huku huweza kumsababishia mwanamke kuingia kwenye kusongeka sana au kumwingiza kwenye kujichukia kunakopindukia mipaka.

Kwa sababu ya kutoolewa, mwanamke anakuwa mkali sana, mkorofi sana na mwenye kuwaona wengine wote kama adui zake. 

Lakini wasichokijua wanawake wengi ni kwamba, kupata mume au mtoto siyo jambo ambalo linampa ukamilifu. Hata mwanaume hawezi kukamilishwa na mke na watoto, bali hukamilika mwenyewe kwanza.

 mani kwamba, mtu asipokuwa na ndoa haheshimiwi au asipokuwa na watotohajakamilika, ni ya zamani sana.

Kuna walio kwenye ndoa ambao maisha yao ni magumu na mabaya kiasi kwamba, wanajiuliza ni kitu gani kiliwaingiza huko. Kuna wenye watoto ambao watoto hao wamechukua maisha yao kwa mikono yao.

Mifano ni mingi sana hapa nchini ambapo kuna watoto wamewauwa mama zao kwa sababu mbalimbali. 

Suala hapa siyo ndoa, bali ni mtu mwenyewe anajiamini kwa kiasi gani.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Mzee Mtambuzi

A freelance Journalist and also teaching self-empowerment, positive thinking as a means of creating the life you desire including spirituality. He is writing in Mwananchi Scoop every Wednesday Visa na Mikasa.


Latest Post