Mwigizaji na mchekeshaji kutoka nchini Marekani, Tiffany Haddish amedai kuwa ameanza kuwatambua wale wote waliokuwa wakituma maneno machafu na kumnanga kupitia mitandao ya kijamii.
Haddish ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye mahojiano yake na gazeti la ‘Los Angeles Times’ ambapo aliweka wazi kuwa baada ya kusemwa vibaya na kutishiwa kifo kupitia mitandao ya kijamii wa Instagram aliamua kuajiri mchunguzi wa kidigitali ambapo kufuatiwa na utafiti huo ilibainika kuwa 75% ya vitisho hivyo viliundwa na roboti kutoka Malaysia na Iran.
Aidha, ili kufanikisha hilo Haddish alidai kuwa aliamua kutengeneza akaunti ya uongo ya Instagram ijulikanayo kwa jina la ‘Sarah’ ili kufanikisha kupambana na chuki hizo kwa kukusanya maelezo kutoka kwa watu waliokuwa wakikomenti maneno machafu.
Tiffany Haddish ameonekana katika filamu kama ‘Night School’, ‘Girls Trip’, ‘Bad Trip’, ‘Like a Boss’ hata hivyo anatarajiwa kuonekana katika filamu ya ‘Bad Boys: Ride or Die’ sehemu ya nne iliyoongozwa na Will Smith na Martin Lawrence.
Leave a Reply