Ikiwa zimepita siku kadhaa tangu mahakama nchini Afrika Kusini kumtaja mfanyabiashara, Sydney Munda Gcaba kuwa ndiye aliyewalipa Sh 109 milioni watuhumiwa sita wa mauaji ya aliyekuwa mwanamuziki Kiernan Forbes, maarufu kama AKA, kwa ajili ya kutekeleza mauaji hayo, familia ya mtuhumiwa imetoa tamko.
Familia ya Gcaba imesema pesa zilizowekwa kwenye akaunti ya benki ya mmoja wa watu wanaotuhumiwa kumuua AKA, ziliwekwa kwa madhumuni ya kibiashara na siyo kwa ajili ya kutekeleza mauaji ya rapa huo.
Kwa mujibu wa News24 iliripoti kuwa Februari 11, 2023 saa sita mchana mmoja wa waliohusishwa na kifo ya AKA, aliyefahamika kwa jina la Gwabeni alipokea pesa kwenye akaunti yake na kudaiwa kuzitoa na kugawana na washirika wenziye.
Hata hivyo taarifa iliyotolewa kwa niaba ya familia ya mtuhumiwa siku ya Jumapili, Mandla Gcaba alisema Gcaba ambaye alitajwa kuwa aliweka sh.Milioni 109 kwenye akaunti ya benki ya mfanyabiashara Gwabeni, ilikuwa kwa ajili ya biashara na si vinginevyo.
Ikumbukwe kuwa AKA alifariki kwa kupigwa risasi February 10, mwaka jana akiwa nje ya mgahawa mjini Durban, Afrika Kusini.
Washukiwa waliyokamatwa wiki kadhaa zilizopita kwa kuhusishwa na kifo chake walikuwa ni Siyanda Myeza (21), Lindokuhle Ndimande (29), Lindani Ndimande (35), ambao ni mtu na kaka yake, Lindokuhle Thabani (30) na Mziwethemba Myeza (36).
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply