Afariki baada ya kula samaki mwenye sumu

Afariki baada ya kula samaki mwenye sumu


Mwanamme mmoja kutoka nchini #Brazil, aliyefahamika kwa jina la Magno Sergio Gomes (46) ameripotiwa kufariki baada ya kula samaki mwenye sumu aina na ‘#pufferfish’ aliyoletewa kama zawadi na rafiki yake.

Taarifa ya kifo cha mwanaume huyo ilitolewa na Dada yake Myrian Gomes Lopes, ambapo alieleza kuwa kaka yake hakuwa mpenzi wa samaki lakini baada ya kula samaki huyo alipata ganzi mdomoni baada ya kukimbizwa Hospitalini ndipo ikagundulika kuwa ganzi ilienea mwili mzima na kusababisha mshtuko wa moyo uliopelekea kifo.

Kulingana na kituo cha Udhibiti wa Magonjwa cha #Marekani, iligundulika kuwa #samaki huyo alikuwa na #Sumu aina ya ‘Tetrodotoxin’ inayopatikana katika inni la #Pufferfish na #Blowfish, samaki hao hutumia sumu hiyo kujilinda dhidi ya wanyama wakali.

#Tetrodotoxin ni sumu hatari zaidi ya mara 1,000 na haina dawa inapotumiwa nyingi huzuia upitishaji wa ishara kutoka kwa mishipa hadi kwenye misuli, na kusababisha kupooza kwa misuli na kupelekea kufa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post