Fahamu zaidi kuhusiana na kufanya biashara ya vinjwaji

Fahamu zaidi kuhusiana na kufanya biashara ya vinjwaji

Mambo vipi ni matumaini yangu mko good kabisa, sasa leo kwenye biashara tumekusogezea kitu konki kabisa. Weeeeh! Kuna baadhi ya watu wanalinifata niwaeleze kuhusiana na biashara za kuuza vinywaji.

Kwa upande wangu sio kama najua sana kuhusiana na biashara hii lakini inabidi nieleze klile ninacho kifahamu kuhusiana na biashara hii

Vinywaji vina soko la uhakika, mahitaji ya vinywaji (kuanzia soda, juice, maji, pombe nk) ni makubwa sana iwe majumbani, maofisini, kwenye migahawa, kumbi za sherehe na uhakika wa kuuza ni mkubwa mno, kwasababu watu watu wengi siku hizi watuwezi kuishi bila kupata kimiminika.

Sasa tuanze wafanyabiashara wenzangu, Mtaji, uzuri wa biashara hii unaweza kuanza biashara kulingana na hela uliyo nayo.  Uwe na mtaji mkubwa sana, mtaji wa kati, mtaji wa chini, au mtaji wa chini kabisa) bidii yako ndio kitu kitakacho fanya biashara yako ikuwe.

Bidhaa za vinywaji zinapatikana kiurahisi na wazalishaji ni wengi pia kuna bidhaa za aina nyingi sana, hivyo una uhuru mkubwa kuchagua kuuza kampuni gani.

Wacha tuzungumzie dondoo muhimu za kuzingatia ukitaka kufanya biashara ya vinywaji.

  • Location/ sehemu utakayo fanyia biashara yako

Kwenye biashara kitu muhimu sana ni “location” lazima uchague eneo la biashara ambalo limechangamka na lina watu wengi, ambapo unaweza kuuza vinywaji vingi na kwa haraka hapo faida itakuwepo. Mfano sehemu ambayo inamzunguko wa watu kama vile, Mbezi, Kariakoo, Makumbusho Stand nk.

  • Mtaji

Mtaji wako ndio unaweza kuamua ufanye biashara ya vinywaji jumla au rejareja, vyote viwili bado unaweza kutengeneza biashara ya uhakika.

Kwanza: Kuuza vinywaji rejareja, lazima vinywaji viwe vya baridi na mtaji wako ukiruhusu tafuta Frem nzuri na tengeneza mazingira mazuri ambapo wateja watakaa na kupata vinywaji kwa utulivu, haijalishi eneo ni dogo au kubwa muhimu weka mazingira mazuri pia unaweza weka na vitafunwa, like bites hata huduma ya chakula na chipsi.

Pia tafuta duka la jumla lililo Karibu na wewe ili uweze nunua vinywaji kwa urahisi au depot, pia unaweza kununua kwa wasambazaji wale wanao sambaza kutumia magari wanakuletea vinywaji hadi katika biashara yako.

Pili: Ukiamua kuuza Kwa jumla basi mtaji lazima uwe mkubwa au wa kati. Hivyo hapa kitu muhimu cha kufanya kabla ya kuanza biashara ni kukusanya taarifa muhimu lazima ujue mahali utakapo fanya biashara soko lipoje, vinywaji gani hasa watu wanataka, jinsi ya kuwasambazia wateja wako, pia tembelea ofisi za wazalishaji wa vinywaji mfano Azam, Mo, Coca Cola, Pepsi na wengine uweze pata taarifa sahihi.

Kuhusu bei ya bidhaa, watakuletea vipi mzigo, pia watakusaidia kukuelekeza jinsi biashara hii inavyoendeshwa kitu ambacho ni muhimu sana kwako. Fanya utafiti wa kutosha kabla haujaamua kuwekeza hela yako.

Tatu: Tangaza biashara yako iweze kujulikana na kufahamika uweze kupata wateja wengi zaidi. Tangaza kwenye mitandao ya kijamii na kila kona yaani uhakikishe wanazengo wanapata taarifa ya duka lako lilipo na bidhaa unazouza. Hata kumlipa Juma Lokole akutangazie wewe mlipe utakuja kunishukuru baadae.

Cha kuzingatia kwenye biashara hii na biashara nyingine yoyote na hii naizungumza kila siku ni kukumbuka biashara inahitaji bidii na ubunifu, hivyo ukitaka kufanya biashara hii tumia muda wako kufanya utafiti na kujifunza zaidi ili ukianza biashara yako uwe na uelewa wa kutosha pia uwe na plan yako usikurupuke.

 






Comments 1


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post